Alain Traore(katikati) akishangilia na wenzake baada ya kuisawazishia timu yake bao katika mechi iliyoisha kwa sare Nigeria 1-1 Burkina Faso (picha na Daily Mail)
Vincent Enyeama golikipa wa Nigeria alishindwa kuzuia mpira uliopigwa na Alain Traore na kubaki akilalama kwa kushika nyasi tupu.(Picha na Daily Mail)
Ahmed Musa(kushoto) akimtoka mchezaji wa Burkina Faso katika mechi ilyotawaliwa na Nigeria.(Picha na Daily Mail)
Emmanuel Emenike akishangilia baada ya kuifungia Nigeria bao huku akiwaacha golikipa na beki wa Burkina Faso wakiwa hawaamini macho yao.(Picha na Daily Mail)
Shabiki wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso akiwa amejipamba na kupendeza vilivyo katika pambano na Nigeria.
.............
Nigeria imeanza kampeini yake ya kinyang'anyiro cha kuwania kombe la
Mataifa ya Afrika, nchini Afrika Kusini kwa kutoka sare ya kufungana bao
moja kwa moja na Burkina Faso katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi C.
Nigeria
ilipata bao hilo muhimu na la ushindi kupitia kwa msahmbulizi wake
Emmanuel Emenike, anayeichezea klabu ya Spartak Moscow ya Urussi kunako
dakika ya 23.
Kikosi hicho cha Super Eagles, kilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.
Baada ya dakika za kwanza 45, zilimalizika huku Nigeria ikiwa kifua mbele kwa bao moja kwa bila.
Awali Nahodha wa Nigeria Joseph Yobo alisema
kushinda kombe hilo sio kazi rahisi, ila wamejitolea kucheza kadri ya
uwezo wao, kuhakikisha kuwa Nigeria, inaibuka mshindi.
Amesema dhamira yao kuu, ni kufikiria hatua za robo na nusu fainali.
Mcheza kiungo, Victor Moses ambaye anaiakilisha
Nigeria kwa mara ya kwanza naye anasema wamejianda vyema na ana
matarajio makubwa kuwa watafanya vyema katika mashindano ya mwaka huu.
Matumaini ya kocha wa Super Eagles, Stephen
Keshi, ambaye anaiongoza timu kwa mara ya kwanza katika fainali hizo ya
kuandikisha ushindi wake wa kwanza ulitumbukia nyongo pale Burkina Faso
iliposawazisha katika dakika za ziada.
Timu zote katika kundi hilo, Ethiopia, Burkina Faso, Nigeria na Zambia sasa zina alama moja kila mmoja.
Nigeria sasa itachuana na Zambia katika mechi yao ijayo kisha icheza na Ethiopia mechi yao ya mwisho ya makundi.
Burkina Faso nayo imeratibiwa kucheza na Ethiopia mechi ijayo kisha ikamilishe kampeinin yake ya raundi ya kwanza na Zambia.
HABARI NA BBC SWAHILI





Post a Comment