Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CHADEMA WAKO KILOSA WAKIVUNA WANACHAMA


Vuguvugu la mabadilikolinaloongozwa na CHADEMA imeonekana kutikisa chama cha wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi sana wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa mkutano Mkuu CUF Taifa Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi katika CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

CHADEMA kimekuwa mara kwa mara kikisigishana na vyama vingine kutokana na vuguvugu hili Mfano ni Pale Katibu wa Itikadi na Uenezi ,Ndg.Nape Nnauye alipowashutumu CHADEMA kuwa wana njama za kuuza nchi kwa mataifa tajiri

Shutuma hizo zilijibiwa vikali na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi,Mh.John Mnyika.

CHADEMA walianza mikutano yao hiyo kwa kuzuiwa na jeshi la Polisi Mkoani Morogoro na baadae kuruhusiwa kuanza mikutano hiyo. 

Kwa sasa imekuwa ikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini huku mkoa wa Morogoro ukiwa unaendelea kwa operesheni hiyo kuongozwa na viongozi wa kitaifa
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top