Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUTOKA IKULU LEO: NGUZA VICKING '' BABU SEYA'' NA ''PAPII KOCHA WAMSHUKURU RAIS DK.JOHN POMBE MAGUFULI

Rais akiwa ameshikana Mikono na kuomba dua na Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson “Papii Kocha”, Francis na Michael walipofika Ikulu jijini leo kumshukuru kwa msamaha wake aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia.

PICHA NA IKULU
Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza leo wamefika Ikulu kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani.
,,,,,,,,,,
Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu"- Babu Seya.

RAIS DK.JOHN POMBE MAGUFULI AOMBOLEZA MSIBA WA MKE WA NAIBU WAZIRI KANGI LUGOLA

Rais Dk. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na mkewe Mary Lugola.

Mke wa Lugola ambaye alikuwa ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Polisi Reli, amekutwa na mauti hayo jana, Januari Mosi, 2018 katika Hospitali ya Rabinisia Memorial iliyopo maeneo ya Tegeta.

Picha na IKULU

BREAKING NEWS: FIFA KUKUTANA TANZANIAShirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiteua Tanzania kufanyia mkutano wake mkuu wa kila mwaka utakaoshirikisha mataifa 19, ukiongozwa na Rais wake Gianni Infatinho.


Mkutano huo mkubwa na wa kihistoria umepangwa kufanyika tarehe Februari 22 mwaka huu katika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Rais Wallace Karia aliyezungumza na wanahabari hivi punde amesema mkutano huo utakuwa ajenda tofauti ikiwemo namna ya utoaji wa fedha za kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.

Karia amesema ajenda nyingine ni pamoja na kuangalia changamoto za usajili wa wachezaji kwa njia mtandao (TMS), kalenda ya kimataifa ya pamoja na nchi wanachama kuwa na vipaumbele vya FIFA.

Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais wa FIFA Giann Infatino na miongoni mwa viongozi watakaohudhuria ni katibu mkuu wa FIFA Fatma Samba Diouf Samoura.

Wengine ni sekretarieti nzima ya FIFA pamoja na rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad na sekretariat yake nzima.

Wengine ni sekretarieti nzima ya FIFA pamoja na rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad na sekretariat yake nzima.

Karia amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ni sehemu ya kukidhi vipaumbele vyake na pia ujio huo utasaidia kuitangaza Tanzania kiutalii pamoja na kurahisisha mahusiano ya kisoka

Karia amesema sababu kubwa ya Tanzania kuteuliwa kuwa sehemu ya kufanyia mkutano huo, ni mahusiano mazuri yaliyopo kati ya viongozi wa soka la Tanzania na wale wa FIFA

WAZIRI MKUU ATOA CHANGAMOTO KWA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA YA KILIMO CHA KOROSHO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wanaioishi kwenye mikoa ambayo zao la korosho linastawi wachangamkie kilimo cha zao hilo kwa sababu lina fursa nyingi.
“Mahitaji ya korosho ni makubwa duniani, korosho zinatumika mahotelini na kwenye mikutano mikubwa, zinatumika kwenye ndege, kwa hiyo bei yake lazima iwe kubwa,” alisema.
Ametoa wito huo jana (Jumapili, Desemba 31, 2017) wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”.
Waziri Mkuu alisema anaamini kuwa kijana yoyote mwenye nguvu ya kufanya kazi hawezi kushindwa kulima zao hilo kwa sababu halihitaji uangalizi mkubwa. “Kijana yeyote anaweza kulima zao hili kwa sababu ekari moja ina miche 37 hadi 40. Kuna mtu atashindwa kuangalia miche 37 hadi ikue?” aliuliza.
Waziri Mkuu alisema kilimo cha korosho ni rahisi lakini pia kilimo cha korosho ni rafiki wa mazingira, kwani miti ikikua inatunza mazingira na inasaidia kuleta mvua. Alisema mbali ya mikoa inayolima korosho ya Lindi, Mtwara, Ruvuma Pwani na Tanga, kuna mikoa mingine ambayo udongo wake umepimwa na kubainika kuwa zao hilo linaweza kustawi bila shida. Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Kigoma, Njombe, Songwe na kuongeza kuwa mikoa ya Singida na Manyara iko mbioni kukamilisha uchunguzi wake.
“Leo tumeanza usambazaji wa miche ya bure hapa Ruangwa ambao najua utafuatiwa na wilaya nyingine hapa nchini. Nimeelezwa kwamba mche wenye kutoa mazao mengi ni wa kuanzia miaka mitatu hadi saba, kwa umri huu miche ya korosho inaweza kuchanganywa na mazao mengine kama ambavyo mtashauriwa na maafisa kilimo ili wakati wa palizi ya hayo mazao, shamba lako la korosho libakie kuwa safi,” alisema.
Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake. 
Mapema, akitoa taarifa ya taarifa ya uzalishaji wa miche ya mikorosho msimu wa 2017/18 mkoani Lindi, Katibu Tawala wa mkoa huo, Bw. Ramadhani Kaswa alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika msimu wa 2016/2017, mkoa huo uliweka lengo la kuzalisha na kupanda miche 1,000,000 ya mikorosho.
“Hadi mwisho wa msimu huu, jumla miche 716,532 ilizalishwa na kusambazwa kwa wakulima sawa na asilimia 71.6 ya lengo lililowekwa. Kati ya hiyo, Halmashauri ya Kilwa ilizalisha miche 55,000, Halmashauri ya Lindi miche 100,000, Manispaa ya Lindi miche 50,000; Halmashauri ya Liwale miche 106,000; Halmashauri ya Nachingwea miche 227,670 na halmashauri ya Ruangwa miche 177,862,” alisema.
“Miche hii iligawanywa kwa wakulima bure ambao walipanda kwenye mashamba yao. Zoezi la tathmini ya miche iliyokua baada ya kupandwa linaendelea kwenye halmashauri zote za mkoa,” aliongeza.
Bw. Kaswa alisema kutofikiwa kwa lengo hilo kumechangiwa na kutopatikana kwa mahitaji yote ya mbegu na vifaa vya uzalishaji, kuchelewa kwa vifaa, na mwamko mdogo wa vikundi vya uzalishaji. Alisema kwa msimu huu wa 2017/2018, mkoa uliweka lengo la kuzalisha miche ya mikorosho iliyobebeshwa na isiyobebeshwa 7,132,000. Kati ya hiyo, Wilaya ya Kilwa walilenga miche 1,122,000, Lindi Vijijini 1,550,000, manispaa ya Lindi 1,000,000, Liwale miche 450,000, Nachingwea miche 1,810,000 na Ruangwa miche 1,200,000.
“Hadi kufikia tarehe 29 Desemba, 2017 tayari miche 4,974,425 ilikuwa imezalishwa na iko tayari kwa kupandwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa kama ifuatavyo:- Kilwa miche 772,000, Lindi Vijijini 1,160,455, manispaa ya Lindi 771,440, Liwale miche 266,000, Nachingwea 991,070 na halmashuri ya Ruangwa imezalisha miche 1,013,460,” alisema.
Sherehe hizo za uzinduzi wa upandaji miche mipya zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya, baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki uzinduzi huo.

CHANZO:Michuzi Blog.

CALL FOR PAPERS: INTERNATIONAL DOCTORAL RESEARCH SCHOLAR’S JOURNAL (IDRSJ) FEBRUARY, 2018 EDITION

CALL FOR PAPERS: CIFCA-JOURNAL OF ISLAMIC BANKING ANDFINANCE (CIFCA-JIBF) Main theme: “ A Decade of Establishing Islamic Banking andFinance Systemin Tanzania: Where are we ?

INVINTATION TO APPLY FOR THE RECOGNITION OF PRIOR LEARNING (RPL) EXAMINATIONS AS A PRE-REQUEISITE TO JOIN DEGREE PROGRAMMES INTO HIGHER LEARNING INSTITUTIONS FOR ACADEMIC YEAR 2017/2018.


FROMA TCU:CHANGE OF PROCEDURE FOR ADMISSIONS TO UNDERGRADUATE PROGRAMMES FOR THE 2017/18 ACADEMIC YEAR


POLISI WAMKAMATA TUNDU LISSU(MB) AKIWA NYUMBANI KWAKE DODOMAUjumbe wa Lissu:
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.

Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.

Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.

Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.

Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa.

Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.

Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.
All the best.

TL 


Source:Jf 

BEI YA NYANYA YAPAA SOKONIBei ya nyanya katika masoko mbalimbali Jijini Dar es Salaam imepanda kulinganishwa na hali ilivyokuwa wiki mbili zilizopita.

Kwasasa bei ya jumla imepanda kutoka shilingi elfu 35 kwa sanduku na kufikia shilingi elfu 60 tofauti na hali ilivyokuwa nyuma.

Baadhi ya madalali wamesema kuwa bei imepanda kutokana na kiasi kidogo cha shehena ya nyanya kinachoingia sokoni hapo kwa sasa wanategemea nyanya kutoka kwa wakulima wa Arusha, Iringa na Makambako pekee.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wanaouza nyanya kupitia vipimo vya asili maarufu kama sado, wamesema kupanda kwa bei kumefanya biashara kuwa ngumu kwani wateja wamekuwa hawamudu ongezeko hilo la bei.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top