Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Picha: Mkubwa Fella aweka hadharani nyumba 5 za kundi la Yamoto Band.




Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima.
Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima.
 
MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band na kuwataka wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji nyumba na sio magari.
Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa wasanii, kwani hii si mara ya kwanza kuwazawadia nyumba wasanii wake. Amesema ameziweka  hadharani baada ya maneno kuzuka kuwa wasanii wa Yamoto Band hawafaidiki na kazi wanazofanya
.
Chanzo: MichuziJr

20% KURUDI KIVINGINE KUACHIA NGOMA MPYA JULAI 18

Msanii mkongwe wa muziki, Abbas Hamisi Kinzasa ‘20%’ amerudi katika label yake ya zamani ‘Combination Sound’ inayosimamiwa na mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Man Water.
Man Water

20% akisaini mkataba mbele ya Man Water pamoja na mwanasheria


Muimbaji huyo ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Award (KTMA) kwa mara moja, huku producer wake Man Water akichukua tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi ngoma kadhaa chini ya producer huyo.


Kupitia instagram, Man Water ameandika: Twenty Percent is back 2016, kaa mkao wa kula ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua, kila kitu kiko sawa sasa, new page.

20% kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake mpya utaotoka Julai 18 mwaka huu huku akijapanga kuandaa albamu yake iitwayo ‘Sauti ya Gharama’.

ANGALIA REKODI ZA JOSE MOURINHO DHIDI YA GUARDIOLA, WENGER, RANIERI, KLOPP, POCHETTINO NA CONTE

Mourinho vs other 3
Jose Mourinho ameteuliwa kuwa kocha wa mpya wa Manchester United na sasa akili zote za watu zina shauku ya kuona namna msimu ujao wa ligi ya England utakavyokuwa.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, ameteuliwa kwa kazi maalum ya kuirejesha United kwenye mstari baada ya kuwa imepotea kwa takriban misimu mitatu mfululizo chini David Moyes na Louis van Gaal ambaye ametimuliwa hivi karibuni. Lakini licha ya ukweli kwamba Jose Mourinho anatambulika kuwa na ushawishi kwenye timu nyingi alizopita hivyo kuchagiza matokeo mazuri, lakini kibarua chake kipya hakitakuwa rahisi hata kidogo.
Mourinho anaenda kukumbana na changamoto kubwa sana. Anakutana tena na mpinzani wake wa La Liga Pep Guardiola anayekuja Manchester City, Arsene Wenger wa Arsenal na Claudio Ranieri wa Leicester. Pia kuna Jurgen Klopp wa Liverpool, Mauricio Pochettino wa Tottenham na bila ya kusahau Antonio Conte ambaye anakuja Chelsea.
Mtandao wa Sky Sports umetoa rekodi za head-to-head za Mourinho dhidi ya makocha wenzake vigogo wa Ligi ya England.
Mourinho v Guardiola
Uhasama kati ya Mourinho na Guardiola ulianza wakati akiwa Inter Milan, pindi walipokutana katika nusu fainali ya Champions League mwaka 2010 wakati huo Guardiola akiinoa Barcelona.
Baadaye msimu uliofuata Mourinho alijiunga na Madrid na kukaribishwa na kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Barcelona iliyokuwa chini ya Guardiola, baadaye kupata ushindi wa 1-0 katika fainali ya Copa del Rey na kubeba ndoo.
Kwa ujumla, Guardiola ana rekodi nzuri mbele ya Mourinho pale timu zao zinakutana katika michuano tofauti. Kati ya michezo 16 waliyokutana Mourinho ameshinda michezo mitatu tu. Hivyo Mourinho atakuwa akipambana kuhakikisha anaondoa rekodi hiyo mbovu .
Mourinho v Wenger
Mourinho atakuwa na fursa nyingine ya kukutana na Arsene Wenger. Wawili hao wamekuwa wakiingia katika migongano ya vita ya maneno tangu mwaka 2004 na vita hiyo kufukia kilele kibaya mwaka 2014 pale wawili hao waliposhikana mashati wakati timu zao zikipambana kunako dimba la Stamford Bridge.
Katika suala zima la matokeo mazuri, Mourinho amemtawala sana mpinzani wake. Hajawahi kufungwa na Wenger katika michezo 13 ya ushindani. Kipigo kikubwa kabisa alichwahi kumpa Wenger ni kile cha magoli 6-0 katika dimba la Stamford Bridge wakati huo Wenger akiadhimisha kutimiza michezo 1000 akiwa kama kocha wa Arsenal.
Ushindi wa Arsenal wa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2015, ulikuwa ndiyo pekee ambao Wenger anaweza kujivunia, lakini Mourinho bado atakuwa na shauku ya kutopoteza mchezo wowote wa ushindani dhidi ya mpinzani wake huyo na kuendeleza rekodi ya kutofungwa.
Mourinho v Klopp
Real Madrid chini ya Mourinho ilikutana na Borussia Dortmund ya Jurgen Klopp mara nne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu wa 2012/13. Katika michezo yote waliyokutana, Klopp aliibuka kidedea, akishinda michezo yake kwenye hatua ya makundi na vile vile kumtupa nje katika hatua ya nusu fainali, shukrani za pekee ziende kwa Robert Lewandowski ambaye alipiga zote nne.
Wawili hao pia walikutana Ligi kuu England mwaka jana ambapo Klopp akiwa na Liverpool aliiadhibu Chelsea ya Mourinho kwa mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika Stamford Bridge.
Mourinho v Pochettino
 
Mourinho amekutana na Pochettino wakati akiinoa Espanyol mara wakati huo akiifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 mpaka 2013. Katika michezo hiyo Mourinho alishinda mara nne na kutoa sare mara mbili.
Pia walikutana mara nne wakati Mourinho akiwa Chelsea na Pochettino akiwa Tottenham. Kwenye mchezo wao wa kwanza, Mourinho alishinda 3-0 na kumfunga katika fainali ya Capital One Cup. Lakini Mourinho alikuja kupata kipigo kitakatifu cha mabao 5-3 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa kwenye dimba la White Hart Lane
Mwezi November mwaka jana, wawili hao walikutana tena na kutoa suluhu kabla ya Mourinho kutimuliwa Chelsea.
Mourinho v Ranieri
Mourinho alichukua mikoba ya Ranieri Chelsea mwaka 2004. Lakini iliwachukua takriban miaka minne pale walipokutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/09. Mwaka huo, Mourinho wakati akiinoa Inter aliibuka na ushindi dhidi ya Juve ya Ranieri.
Katika msimu huo Juventus walimaliza katika nafasi ya pili, na Ranieri akaenda Roma. Mourinho wakati huo bado akiinoa Inter hakushinda kwenye michezo yote miwili ya Sirie A dhidi ya  Roma ya Ranieri, lakini alifanikiwa kumfunga 1-0 Ranieri katika fainali 1-0 ya kombe la Coppa Italia.
Miaka mitano baadaye wawili hao wanakutana Mourinho akiwa tena Chelsea huku Ranieri akiinoa Leicester. Wamekutana mara moja na Leicester kuifunga Chelsea kwa magoli 2-1 December mwaka jana. Huo ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Mourinho kabla ya kutimuliwa, na hatimaye Ranieri alifanikiwa  kubeba taji lake la kwanza akiwa nchini England.
Mourinho v Conte
Mourinho amekutana na Conte mara moja tu. Ilikuwa ni December mwaka 2009 wakati Inter ya Mourinho ilipomenyana na Atalanta ambayo ilikuwa chini ya Conte na mchezo kumalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1. Baada ya hapo hawajawahi kukutana tena.

PICHA LIVE ZA MASTAA SHILOLE NA VANESA MDEE WALIVYOPIGA SHOO YA PAMOJA JANA USIKU




Dakika chache kabla ya Show Vanessa Mdee akiwa backstage alinukuliwa akisema“Kiukweli haukuwa ugomvi bali tulijaribu kuwaonesha watu kuwa usiamini kila unachokiona kwenye mitandao, namuheshimu sana Shilole katika kazi zake, lakini baada ya sisi kufanya vile watu walionekana kama wanataka kuona sisi tukigombana”

Huenda wewe ulikuwa ni moja kati ya watu waliokuwa wameshtushwa na taarifazilizokuwa zimeenea wiki mbili zilizopita kuwa Vanessa Mdee na Shilole wana bifu, ukweli umejulikana usiku wa May 29 2016, kuwa haikuwa bifu bali ni promo ya show yao ya pamoja waliofanya usiku huo.














Vanessa alimsurprise Shilole On Stage kwa kumletea zawadi ya ugali kwenye stage kumuonyesha yeyey ni mtoto wa ugali ndondo.







Hakuna cha bifu wala nini sie ni kazi tu hapa ,, ni kama ndivyo wanavyosema V Money na Shishi baby.

MJ Records Wazungumzia Ukweli Kuhusu Wimbo Freedom Ulioleta Mgogoro Kati ya Sugu na Mr Blue

Mr Blue analalamika kuwa Sugu ameupora wimbo wake ‘Freedom’ aliokuwa amemshirikisha kwa kutoa verse zake na kuufanyia video iliyotoka jana.

Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. MJ Records walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.

Producer mkuu wa studio hiyo, Marco Chali ameiambia Bongo5 kuwa beat ya wimbo huo ilitengenezwa na mdogo wake, Daxo Chali aliyetengeneza chorus yake na alimpa msanii wake Lizzy aliyeingiza.

“Ngoma ilikuwa ipo tayari na ilikuwa inasubiria verse tu kadhaa halafu ilikuwa ni ngoma yake [Daxo]. Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa akasema atamshirikisha Mr Two,” amesema Marco.

Walipoifanya, Blue aliiamua kuiachia kupitia Mkito peke yake kwa maana kwamba hakuiachia ngoma rasmi. Anasema baada ya muda Sugu alimpigia simu kumuomba kuwa afanye version nyingine ya wimbo huo na aifanyie kabisa na video.

Anadai alimuambia Sugu aongee na Daxo waliyekubali kuufanya tena hadi video ikafanyika huku yeye [Marco] akiwa hajui chochote kilichoendelea baada ya hapo. Na Marco anasema pia hakuhusika kwenye uingizaji wa sauti zote mbili zaidi ya kuzifanyia mixing peke yake.

Marco amesema anadhani wawili hao [Sugu na Blue] waliongea kuhusu hatua hiyo na kwamba wao kama studio hawakuwa na kipingamizi chochote kuhusu kurudiwa kwa wimbo huo kwasababu walitaka wimbo ufike mahali.

Hata hivyo Marco amedai kuwa wote wawili [Sugu na Blue] hawakulipia wimbo huo na kwamba MJ Records iliwapa kwasababu ya ‘love’ tu. Marco anasema anashangaa kuona Mr Blue sasa hivi anatoa malalamiko hayo.

“Ni kwasababu mimi nilipenda tu kutoa studio bure kwanini usijitahidi ukapeleka hiyo nyimbo ikafika sehemu ikafahamika, at least pia akili za watu zilizotumika watu wazione. Na ndio hicho kitu naona ni kizuri, yeye kwa mfano angefanya hata video, sidhani kama Sugu angerudia huo wimbo,” ameongeza Marco.

“Na yeye aliposema kwamba anataka afanye video, namaanisha kwamba walishaongea na Blue kwamba yeye afanye video. Halafu Daxo wasije kumweka tena kwenye matatizo akaonekana kwamba ni producer mzinguaji ni vitu ambavyo havitamsababishia biashara na dogo mwenyewe ndio anataka kutoka. Na anajua wazi kuwa ni watu wazima wameongea kule,” amesisitiza Marco.

Kwa upande wake Daxo Chali amethibitisha alichosema kaka yake.

“Mr Blue Hajanilipa Hela Yoyote Kama Hilo Swala Ndio Mnataka Kujua , Na Mr Blue Na Sugu Wote Wameikuta Beat Studio Ikiwa Na Chorus Ambayo Mimi Ndio NimeAndika Na Kumuweka Msanii Wangu Na Idea Ya Wimbo Ni Ya Kwangu Pia,” ameandika kwenye post yangu ya Instagram.

“So Mr Blue Hakuiwekea Mkazo FREEDOM Then Sugu Akaomba Afanye Version Yake. Mimi Sioni Kama Kuna Tatizo Hapo, Labda Kama Angefanya Msanii Ambaye Hayupo Kwenye Wimbo Wa Kwanza. Wamalize Tofauti Zao Tu.”

Naye Sugu amedaiwa kujibu malalamiko ya Blue kwa ujumbe huo chini kwenye WhatsApp

UBUYU MPYA MJINI TEAM ZARI WALA SAHANI MOJA NA MREMBO ANAYEDAIWA KUTOKA NA BABA TIFFAH

Kuna ubuyu mpya mjini… Na tena unaonesha umepata wateja wengi kwa muda mfupi.
12783337_589751924508095_2021141505_n
Mashabiki wa Zari the Bosslady wanamshambulia Lynn, mrembo aliyetumika kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii wa WCB, Raymond kwasababu wamesikia tetesi kuwa amechepuka na Diamond Platnumz.

Tetesi hizi ni kubwa kiasi ambacho watu walio karibu na mastaa hao wamedai kuwa zimeitikisa ikulu ya Chibu. Wanadai kuwa Zari amekerwa na tetesi hizo na kwamba uhusiano wao umepata dosari. 

12797777_1677553662507605_1408288689_n
Wiki hii tetesi hizo zimevuma zaidi kiasi ambacho mashabiki wa Zari wamekuwa wakimmiminia matusi Lynn kwenye akaunti yake ya Instagram.

Inafurahisha kwasababu Lynn haoneshi kutikiswa na matusi hayo huku pia akipewa support kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawampendi Zari. Of Course Team Wema yote inaonesha kuwa nyuma yake!

Cha kuvutia zaidi ni kuwa Lynn ni msichana mdogo na mrembo sana kiasi ambacho wasiompenda Zari wanasema anafaa zaidi kuwa kifaa cha Bin Mondi. Kwa wengi hizi bado ni tetesi tu lakini kama ukiangalia post za nyumba za Lynn, utagundua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Daimond kwakuwa amekuwa akiweka picha zake [Diamond] mara kwa mara.

Kubwa
10012561_1698384190423397_1266062110_n
Lynn ana kila sababu ya kuwa na wasiwasi sababu kuna mashabiki wanaoenda mbali zaidi kwa vitisho vyao.

“We see these stories going around & we are watching you. Ntakutoa meno. Utak*zwa kwa mk**u since you look like a hor*y bitch jumping on people’s husbands… you have been warned,” ameandika shabiki mmoja.

“Watch your steps. We already have a bajaji which followed you to your house. You like f**ing other people’s men? You will get whats coming to you. Stay away from mama tiffahs man. Ut**wa mal**a ww. Rudi kumpost tena,” ameongeza.

Lynn ana watetezi wengi pia.
“Aisee hata ningekua mimi bwanangu niskie ana mwanamke mzuri kunishinda lazma nitahangaika!! Khaaa si kwa uzuri huu Lynn,” ameandika shabiki mmoja.

“@zarithebosslady rudi kwenu BANANGE kule kijijini ulivoendaga kuroga siku ile basiii!! Ku****yo M***ya la mwaka 79 yani usitake nianze kukupa michambo,sawa? Eti omulunji,ushapewa kiki za kutosha k*** wewe ulikutwa na followers elfu moja sasa hivi una followers milion inaenda milion 2..haya fanya yako bibi la kupenda kiki mpaka linasahau kuwaangalia wanae!! Fanya mitende ile,halafu hukuchomaga kinga ya matende wewe ulivozaliwa eeeh?? Au enzi hizo uganda kinga zilikua bado hazijaingia?”

Hatari tupu! Acha tuone movie hii itaishia wapi! Mfahamu zaidi Lynn kwa picha zake hizo chini.
12917999_205133643196253_42235573_n
12826310_582582971895982_863049660_n
12825945_951472618264887_1178545026_n
12747661_948002948588060_171661368_n
12716961_957459444323031_1514314940_n
12599293_1246832102013248_1544433012_n
12530907_1811460449082622_738820174_n
12328027_865360636925265_1867668250_n
12106002_1729977020569659_275135064_n
10387845_1562611300722919_558593386_n
916042_1003190396431071_463545754_n
12816813_1708656342725657_1025825814_n
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top