Nape Nnauye akielezea kuhusu “Harambee za
Kisanii” za CHADEMA wakati akiongea katika kipindi cha Makutano na Fina Mango
Nape Nnauye katika picha ya pamoja na
watangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango, Musa Kipanya na Mwanasheria
Joseph alieelezea sheria za msajili wa vyama vya siasa.
-------
Jumamosi katika kipindi cha Makutano ndani ya Magic FM
katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye aliongea kuhusu kauli yake kuwa
Harambee za CHADEMA ni za kisanii kwani kuna wafadhili ambao wako nje ya nchi
wanaotumia mwanya huo kukifadhili chama hicho.
Nape alisema kuwa kuna hela chafu zinazoingizwa na Mataifa
yanayotaka kuvuruga siasa na kuwaweka vibaraka ambao watafanya kile wanachotaka
watu hao wanaozimezea mate rasilimali za
nchi husika huku akitolea mfano wa Congo. Aliendelea kusema kuwa kuna pesa
chafu ambazo zinaingizwa toka nje na kuchangiwa katika harambee na watu
wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa.
Nape amewataka chadema kutoa majina ya
watu waliowachangia na kazi wanazozifanya ili jamii iwatambue. Alipoulizwa kama
anayafahamu majina ya wafadhili wa nje wa chadema kwa nini asiyataje Nape
alijibu katika siasa kuna kitu kinaitwa “Timing” kwamba anasubiria wakati
muafaka huku akitolea mfano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alieitaka
Serikali iwataje vigogo wanaomiliki mabilioni katika mabenki ya nje ya nchi la
sivyo atawataja. Alimaliza kwa kutaka kila mtu ahakikishe anapigania amani ya
nchi.
Post a Comment