Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.
Gladyness Mkamba (katikati) akizungumza wakati akimuwakilisha Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Meja Gen. Gaudence Milanzi katika ufunguzi wa
Mkutano wa mapitio ya kukamilisha mradi wa Kitaifa wa Uendelezaji Misitu
na Ufugaji Nyuki nchini (NFBKP II) unaofadhiliwa na Serikali ya Finland
kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika Chuo cha Taifa cha
Utalii Tawi la Bustani Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2016.
Kushoto ni Mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa
nchini Bw. Mikko Leppanen.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tawi la Bustani Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.
Gladyness Mkamba akizungumza na Waandishi wa Habari katika chuo cha
Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2016.
Mratibu
Msaidizi wa mradi wa NFBKP II, Bi. Magdalena Muya (kulia) akiwasilisha
mada ya jumla juu ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2013 na kukamilika
mwaka huu 2016.
Mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen akieleza jambo kwa waandishi wa habari.
Picha ya pamoja.
Na Hamza Temba, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii
JAMII
hapa nchini imeaswa kutumia fursa iliyopo ya ufugaji wa nyuki na
upandaji wa miti kibiashara kujikwamua kwenye lindi la umasikini.
Hayo
yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya
Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba akizungumza na Waandishi wa
Habari Jijini Dar es Salaam.
Bi.
Mkamba alisema kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kuzalisha asali kwa
wingi duniani ambayo ikitumiwa ipasavyo itasaidia kukuza kipato cha mtu
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
"Kwa
sasa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika ambapo inazalisha asali tani
34,000 kwa mwaka baada ya Ethiopia inayozalisha tani 56,000. Hata hivyo
kiwango hicho ni kidogo kwa kuwa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha asali
tani 1,038,000 kwa mwaka" Alieleza.
Akizungumzia
changamaoto kuu inayosababisha kiwango hicho kisifikiwe kirahisi,
amesema ni utashi hafifu wa jamii kujishuulisha na kazi za ufugaji nyuki
na uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti.
Bi.
Mkamba aliongeza kuwa Jamii ikihamasishwa vya kutosha juu ya faida za
ufugaji nyuki na upandaji wa miti inaweza kutoa matokeo ya haraka kwa
kuwa asali ina faida kubwa ikiwemo za kiafya na za kiuchumi.
Kwa
upande wake Bi. Magdalena Muya ambaye ni Mratibu Msaidizi wa mradi wa
Kitaifa wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameeleza kuwa
changamoto zingine zinazokwamisha mafanikio katika sekta ya ufugaji
nyuki nchini ni ukosefu wa teknolojia za kisasa za ufugaji nyuki na
uzalishaji wa asali pamoja na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha miradi
mikubwa ya ufugaji wa nyuki.
Nae
mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw.
Mikko Leppanen, ameeleza kuwa Misitu ya Tanzania inakabiliwa na
changamoto ya uharibifu mkubwa unaosababishwa na shughuli za kibinadamu
ambapo hupelekea ukame na kuathiri pia uzalishaji wa asali ambao
hutegemea malighafi za misitu.
Mshauri
huyo ameiasa jamii hapa nchini kutunza mazingira ya misitu, kupanda
miti kibiashara na kuhifadhi mazingira ambayo yatasaidia kuweka
mazingira bora ya kuishi ikiwa ni pamoja na kuwezesha ufugaji wa nyuki
kibiashara na kuwainua watu kiuchumi.
Wakati
huo huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili
Bi. Gladyness Mkamba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Meja Gen. Gaudence Milanzi wakati akifungua mkutano
wa siku moja wa mapitio ya kukamilisha Mradi wa Kitaifa wa Misitu na
Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameishukuru Serikali ya Finland kwa
kusaidia ufadhili wa mradi huo.
Ameeleza
kuwa mradi huo ambao bajeti yake ni Euro Milioni 19.5 ambazo ni zaidi
ya Tsh. Bilioni 47 kwasasa unafadhili mpango wa miaka minne wa Misitu
binafsi katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Morogoro kwa lengo la kuinua
kipato cha wananchi wa vijijini katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania,
Mikoa hiyo ni shemu ya Mikoa saba ya jumla inayofadhiliwa na mradi huo.
Amesema
hayo yatafanyika kwa kuanzisha misitu ya uhakika yenye faida na
kuongeza thamani ya mazao yake kwenye mtiririko wa uzalishaji kuanzia
mbegu za miti hadi kwenye bidhaa bora za mbao.
Mradi
huo ulianza Oktoba mwaka 2013 hadi Oktoba 2015 na kuongezewa muda wa
ziada wa miezi minne ambapo unakamilika mwezi huu wa Februari 2016.
Post a Comment