Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WACHUNGAJI WAZIDI KUTIMULIWA KKKT DAYOSISI YA IRINGA,BAADA YA MCHUNGAJI HOPEMAN AMEFUATA MCHUNGAJI MTATIFIKOLO


KAMATI ya Utendaji ya Halmashauri kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania- Dayosisi ya Iringa imemvua uchungaji, Mchungaji Lambet Mtatifikolo.



Mchungaji Mtatifikolo ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Iringa amevuliwa uchungaji kwa madai kwamba amepoteza sifa za uchungaji na za kufundisha wachungaji.



Hata hivyo Mchungaji huyo amepinga maamuzi hayo na amedai kwamba atakwenda mahakamani kuzuia maamuzi hayo endapo uongozi wa kanisa hilo hautayafanyia kazi majibu yake.



“Nimeshawasilian na wakili wangu na nimetaka aanze mara moja kuandaa taratibu za kupinga maamuzi hayo,” Mchungaji Mtatifikolo alisema.



Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Owdenburg Mdegella (nakala tunayo) iliyotumwa kwa mchungaji huyo, ilimtaka arudishe kanzu, stola, kola, shati jeusi na mshipi wa uchungaji kabla ya Julai 17, mwaka huu.



Pamoja na agizo hilo, Mchungaji Mtatifikolo hajarudisha vifaa hivyo akikisistiza utaratibu haukufuatwa wakati akivuliwa nafasi yake hiyo ndani ya Dayosisi hiyo.



Kwa mujibu wa barua hiyo, Kamati hiyo iliketi Juni 27, mwaka huu na kuazimia kwamba kuanzia Julai 3, mwaka huu, Mchungaji Mtatifikolo asiendelee na shughuli za kiuchungaji katika dayosisi hiyo kwasababu hizo.



Azimio hilo limetumwa kwa maafisa wote wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Iringa na wakuu wote wa majimbo wanaotakiwa wasimualike kuhudumu neno na sakramenti au kusimamia ubatizo na ndoa na pia asipewe uongozi wowote ndani ya kanisa.



Hata hivyo katika barua yake kwenda kwa Askofu Dk Mdegella na nakala yake kutumwa kwa Mkuu wa Kanisa la KKKT, Maaskofu wote wa KKKT, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Iringa, maafisa wa KKKT Dayosis ya Iringa na wakuu wote wa majimbo, Mchungaji Mtatifikolo amekataa maamuzi yaliyofanyika dhidi yake na kikao hicho.



Mchungaji Mtatifikolo amesema hakuna ushahidi ulioainishwa ukimuonesha kwamba amekosa sifa za kuwa mchungaji katika dayosisi hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka kumi.



“Maamuzi hayo yamefanyika pia bila kufuata taratibu za kisheria kama sheria ya kazi na sheria ya ajira na mahusiano kazini, na huduma za kazi,” inasomeka sehemu ya barua yake.



Katika utetezi wake wa kupinga maamuzi hayo, Mtatifikolo amesema kamati ya utendaji ilifikia maamuzi hayo kwa kusikiliza upande mmoja kinyume na taratibu za kanisa, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zilizotajwa hapo juu.



Kwa kuzingatia hayo, Mtatifikolo amesema haafiki uamuzi huo mpaka pale mpaka dayosisi hiyo itakapoweza kuthibitisha hoja zake.
Kwa Habri zaidi Bofya:http://www.frankleonard.blogspot.com/

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top