Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MRAGHABISHI MAIMUNA SAIDI AGEUKA SHUJAA WA KIJIJI CHA MWIME KAHAMA

Na Krantz Mwantepele ,       
Ziara niliyofanya katika Kijiji cha Mwime kata ya Mwendakulima  wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mwishoni wa  mwezi Novemba mwaka huu ,ilinipa mwanga wa jinsi ambavyo wananchi wakiamua kuchukua hatua wanaweza kubadili mfumo mzima na kuweza kujiletea maendeleo katika Nyanja zote za maendeleo .Kijiji cha Mwime ambacho wananchi wengi wanajihusisha na biashara, uchimbaji wa madini na kilimo cha pamba na wapo katika eneo ambalo Barick Buzwagi wanafanya uchimbaji mkubwa wa dhahabu.
Ofisi za   kijiji hicho cha Mwime kilichopo kata ya Mwendakulima wilayani Kahama 
Mgogoro wa Maslahi wa wananchi wanaozunguka mgodi uliokuwa unamilikiwa na Barrick na sasa Accaccia uliopo  wa Buzwagi kwenye wilaya ya Kahama katika kijiji cha Mwime kilichopo kata ya Mwendamkulima  katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Unaibua mashujaa wa kutetea haki na kudai uwajibikaji u wa viongozi katika kuendeleza utawala bora na maendeleo kwa ujumla lakini mwishoni inageuka kuonekana ni maadui wa maendeleo . 
Kwa muda wa miaka zaidi ya mitano  sasa kijiji hiki kimekuwa katika pilikapilika za kuhakikisha wan-aendelea kunufaika na rasilimali yao ya madini ya dhahabu ambayo kwa sasa yanachimbwa na kampuni ya Accacia  katika mgodi wa Buzwagi kupitia Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba yaliyosainiwa mwaka 2007.
Kwa mujibu wa kifungu  1.1 cha Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea kwa niaba ya Barrick na kijiji; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano baada ya uzalishaji kuanza na kisha pande mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi. Na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huu ulianza rasmi mwaka 2009.

Nikiwa ziarani  wilaya ya Kahama nilitembelea kijiji hiki ambacho mwanzoni mwa mwaka 2007 wananchi wengi wa kijiji cha Mwime na maeneo ya karibu walijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu kabla kampuni ya Pangea kuja kuchukua maeneo hayo kwa kuhodhi mashimo yaliyojulikana kwa majina ya  Zanzibar na majimaji na kuwafanya wakazi hao kuondoka hapo kupisha uchimbaji wa kisasa,
Mategemeo ya wananchi kupata maendeleo makubwa baada ya kampuni ya Pangea kuanza uchimbaji huo wa kisasa yaliendelea kufifia kila uchwao baada ya makubaliano ya kulipwa kiasi cha milioni  60 kila mwaka kwa kipindi cha miaka kipindi cha miaka mitano  cha uchimbaji  wa madini kutotimizwa kwa wakati.Licha ya kutokuwa na uelekezi rasmi wa kiseheria wa makubaliano hayo lakini yaliwafanya  wananchi wa mMwime kuendelea kuishi maisha magumu  licha ya kuwa mgodi wa Buzwagi  kuweza kufanya uchimbaji kwa muda mrefu.
Kuchelewa kwa malipo kama walivyokubaliana kulisababishwa pia na mapungufu ya uongozi wa kijiji kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.Sababu nyingine inayotajwa ni kwa Wanamwime wenyewe kushindwa kudai na kuwahimiza vi-ongozi wao kuchukua hatua kwa kufuatilia suala hilo.

Bi Maimuna akiwa na  mjukuu wake katika duka lake analouza pembejeo za kilimo kwa wakazi wa kijiji cha Mwime
Mraghabishi na mpambanaji wa haki za binadamu Bi Maimuna Saidi ambaye pia ni mwananchi wa kijiji hicho ambaye yeye na wenzake watano  walichukua hatua ya kuanza kuhimiza ufuatiliaji wa pesa hizo kama walivyokubaliana na baada ya mazungumzo marefu na pia ushirikishaji wa wananchi wote wa kijiji kupitia mikutano ya kijiji waliweza kufanikisha upatikanaji wa  ya million 300/ kama malipo ya mwaka 2009 – 2013 .
Mama maimuma saidi (Mwenye kilembo)akitoa  maelezo jinsi gani walivyofanikisha kupatikana kwa maendeleo katika kijiji cha Mwime kutoka katika mgodi wa Buzwagi  kwa baadhi ya waandishi wa habari na wataalamu wa mitandao ya kijamii  niliombatana nao 

 Hivyo Maimuna Said kupitia ufahamu aliopatiwa alimshawishi Diwani mara kwa mara kuweza kuchukua hatua zaidi, kwa kuwa yeye alikuwa na mamlaka zaidi.Na mwishowe kupitia harakati mbalimbali na ushirikishwaji wa wananchi wenzao walifanikiwa  kupata kiasi hicho cha pesa.
Pesa hizo pia zilitumika kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii  kama ujenzi wa miundombinu ya umeme ,nyumba za manesi, nyumba ya kupumzikia wageni kama kitega uchumi lakini haya yote yalikuwa kama kipaumbele cha wananchi kufaidikapia kiasi kilichobaki kulipa baadhi ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao katika upanuzi wa barabara .
Moja ya nyumba zinazojengwa katika kijiji hiki cha Mwime kama moja ya matumizi ya pesa walizopata kutoka katika mgodi wa Buzwagi 
Huu mchakato wote usingeweza kufanikiwa kama Wanamwime wenyewe wasingesimama pamoja na kudai haki yao. Kwa hakika ili tupate tutakachotaka ni lazima tuchukue hatua za dhati pasipo kuchoka wala kukata tamaa huku tukishirikiana na viongozi wetu kwani kuna msemo unasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kama dhana waliotumia wanaMwime  wakafanikiwa katika harakati zao za kujiletea  maendeleo kijijini hapo.

TGDC NA MKAKATI WA UZALISHAJI WA UMEME KUPITIA JOTOARDHI

 Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakiweka saini Mkataba wa wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (kushoto) pamoja na Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara wakikabidhiana Mkataba wa Maelewano (MOU) wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za TGDC zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson, wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirkiano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
KUTOKANA na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati itokanayo na jotoardhi (Geothermal Energy) imetajwa kuwa ni muhimu katika kuepukana na hasara kubwa na isiyo ya lazima inayotokana na matumizi ya mitambo ya mafuta katika kuzalisha umeme na kuifanya Tanzania kuondokana na tatizo la umeme usiokuwa na uhakika pamoja na kuleta maendeleo nchini.
Ili kuleta Maendeleo haya katika sekta ya nishati, Tanzania hainabudi kugeukia katika vyanzo vingine vya uzalishaji umeme ikiwemo nishati hiyo ambayo kwa kutumia mvuke wa maji yaliyochemshwa na joto la asili lililopo chini ya ardhi, nishati ya umeme inaweza kuzalishwa na kukidhi mahitaji ya nishati ambayo yatasaidia kuwa kiunganishi cha ukuaji wa uchumi nchini. 
Tanzania iko katika ukanda wa Bonde la Ufa (Rift Valley), hivyo kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa hifadhi kubwa ya nishati itokanayo na jotoardhi ambayo inaweza kutumika katika uzalishaji wa umeme na kuinua uchumi wan chi yetu.
Nishati hii itakuwa mkombozi kwa taifa letu hususani kwa mwananchi wa kipato cha chini kwani tunaamini kuwa matumizi ya nishati hiyo yatapelekea kupungua kwa gharama za manunuzi ya umeme na kutokana na ukweli kwamba nishati hiyo pindi ipatakinapo haitarajiwi kuisha.
Unafuu wa umeme utakaozalishwa na jotoardhi unatokana na ukweli kwamba mitambo inayotumika kuzalisha umeme huo kuendeshwa kwa mvuke ambao unatokana na majimoto toka ardhini tofauti na uzalishaji wa umeme uliokuwa unatumika kwa kutumia mitambo yenye kutumia mafuta ambayo gharama yake ilikuwa juu kwa Serikali.
Hapa nchini, kuna viashiria vingi vinaonyesha uwepo wa jotoardhi hasa kwa maeneo ya vijijini ambako umeme sehemu nyingi haujafika, kutokana na hilo sasa Serikali yetu hainabudi kutupia macho katika nishati hii kwa kuhakikisha kwamba wananchi ambao wnaaishi maeneo ambayo nishati hiyo inapatikana wananufaika na umeme huo.
Jotoardhi ina matumizi mengi kwa jamii yetu, mfano majimoto yatokayo ardhini yanaweza kutumika katika kukaushia mazao mfano matumizi ya Vitalu shamba(Green Houses) badala ya kutegemea jua. Mwananchi wa kipato wa chini anaweza kutumia majimoto kukausha mazao yake kwa mfano mpunga, maharage, mahindi, karanga katika ubora ule ule kama wa jua. 
Matumizi mengine ya majimoto ni katika kupasha nyumba joto hasa katika wananchi wale waishio mikoa yenye baridi kali kwa kujenga mabomba ya kupitisha maji ya moto ndani ya nyumba zao.
Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) imepewa lengo na Serikali la kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa Megawati 200 na kuuingiza katika gridi ya Taifa kufikia mwaka 2020.
Hivi karibuni, TGDC kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (ESMAP) zilifanya warsha ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam ambayo iliwakutanisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali yanayoshughulikia masuala ya jotoardhi yakiwemo GDC la Kenya, Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), BGR la Ujerumani, ICEIDA la Iceland, Chuo cha Umoja wa Mataifa kinachofundisha nishati ya Jotoardhi (UNU), TNO la Uholanzi pamoja na Shirika la Star Energy la nchini Indonesia ambapo wadau hawa wote wameweza kufanikiwa kuipata nishati hiyo, hivyo watatoa mchango mkubwa kuliwezesha shirika la TGDC kupata mafanikio na hatimaye nishati hiyo kuweza kupatikana.
Katika warsha hiyo, Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji nishati ya Jotoardhi (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe alisema kuwa warsha hiyo inalenga kujadili kwa kina njia mbalimbali zilizotumiwa na baadhi ya mashirika hayo hadi kufanikiwa kupata nishati hiyo ikiwemo uanishaji wa huduma tofauti zifanywazo na mashirika hayo katika kulisaidia shirika la TGDC. 
“Matokeo ya warsha hii tuliyoifanya tumeweza kuwasiliana na wenzetu wa Benki ya Dunia (ESMAP) kwa kukusanya wataalam toka taasisi mbalimbali pamoja na Mashirika mbalimbali ambayo yamewahi kufanya kazi hii ya utafutaji wa nishati ya jotoardhi na lengo letu ni kutaka kufahamu njia ambazo wenzetu walizitumia mpaka kufanikiwa ili na sisi tupate kujifunza”, alisema Njombe.
Mhandisi Njombe aliongeza kuwa warsha hiyo itawezesha rasilimali chache zilizopo ziweze kutumika ipasavyo katika kuleta matokeo ambayo TGDC inatarajia kuyapata ili kuhakikisha kuwa lengo la upatikanaji wa nishati hiyo linafikiwa.
Sambamba na warsha hiyo, Serikali kupitia TGDC na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la nchini Iceland (ICEIDA), wamesaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata Mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi ikiwemo kuwajengea uwezo Wataalam wetu wa hapa nchini pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo.
Makubaliano hayo yalifikiwa Jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson, huku likishuhudiwa na Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Uendelezaji wa Nishati Jadidifu, Bwana Edward Ishengoma pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka TGDC na Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, matarajio ya Tanzania ni kuzalisha kiasi cha megawati 200 za umeme unaotokana na nishati ya jotoardhi ifikapo mwaka 2020, ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa, hazina iliyopo kupitia nishati hiyo ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya umeme wa megawati 5,000, kutokana na nishati ya jotoardhi toka ardhini.
Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, utayari na ushirikiano unaoonyeshwa na nchi ya Iceland kupitia Shirika la ICEIDA itakuwa kichocheo kikubwa kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na nishati ya kutosha ya umeme na kuchochea maendeleo nchini.
“Tuna malengo mengi kupitia nishati hii ya jotoardhi, utafiti ndio njia itakayotufanya kufikia malengo haya, ushirikiano huu ni mwanzo mzuri kwa upande wetu sisi Tanzania, na nafahamu kuwa Iceland mlianzia katika hatua za chini kabisa lakini sasa mko mbali, zoefu wenu katika masuala haya ya nishati hii utatuwezesha kuweza kufika mahali tunapotarajia,” alisema Mhandisi Masanja.
Naye, Mkurugenzi wa ICEIDA, Bwana Engilbert Gudmundsson alieleza juu ya umuhimu wa nishati hiyo na unafuu wake wa gharama ikilinganishwa na nishati nyingine na kueleza kuwa, zaidi ya asilimia 25 ya umeme unaozalishwa nchini Iceland unatokana na nishati ya jotoardhi, hivyo Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya kupata nishati hiyo kwa kuonyesha juhudi zake ikiwemo kushirikiana na ICEIDA.
“Sisi Ilituchukua kipindi cha miaka 25 kufikia mafanikio tuliyonayo katika nishati ya jotoardhi, hivyo kutokana na uzoefu wetu huu hatunabudi kutoa uzoefu wetu kwa TGDC ili kuhakikisha inafakia malengo,” alisema Gudmundsson.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe alishukuru na kuonyesha hali ya utayari wa ICEIDA katika kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia malengo yake ya kuendeleza nishati hiyo, utakaosadia kufanyika kwa tafiti katika maeneo mbalimbali yenye viashiria vya nishati hiyo kama vile maeneo ya Luhoi pamoja na Kibiti Mkoa wa Pwani.
Mhandisi Njombe anabainisha kuwa, kutokana na utafiti utakaofanywa kwa ushirikiano kati ya TGDC na ICEIDA, utawezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na halisi ambazo zitafungua njia ya kupata misaada zaidi kutoka katika taasisi na wahisani mbalimbali ambao wamejikita katika masuala nishati hiyo.
Moja ya hatua mbalimbali ambazo zilizofanywa na TGDC mpaka hivi sasa ni kwamba jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha uzalishaji umeme nchini na kupitia makubaliano hayo, ICEIDA itawezesha Wataalam wa ndani kutoka TGDC kupata ujuzi na uzoefu utakaowezesha kufanyika kwa tafiti nyingine katika maeneo mengine huko mkoani Mbeya.
Katika hatua nyingine TGDC pamoja na Kampuni ya TOSHIBA ya nchini Japan zimetiliana saini Mkataba wa Maelewano wa kufanya tafiti kwa pamoja zinahusu maeneo yenye viashiria ya upatikanaji wa nishati ya jotoardhi.
Utiaji saini wa mkataba ni hatua nzuri ambayo sasa inaliwezesha Shirika la TGDC kuweza kupata msaada wa kitaalam ambao utaliwezesha shirika hilo kuweza kuchimba ardhini kwa lengo la kupata mvuke utakaoweza kuzalisha umeme.
Akiongea wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba huo, Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe alisema kuwa kupitia Serikali ya Japan hususani Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Kampuni ya TOSHIBA watasaidia kuomba ufadhili wa Serikali yao ili kuweza kuendeleza ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine yanayoendana na nishati hiyo.
“Katika utafiti wa nishati ya jotoardhi tunahitaji watu wenye elimu na uzoefu na ujuzi wa kutosha, miongoni mwa makubaliano ndani ya mkataba huu tuliosaini leo ni wafanyakazi wetu kadhaa kuwapeleka nchini Japan kwenye vyuo vyao ili kuweza kupata mafunzo ya darasani na kutembelea maeneo ambayo Japan wana vituo vya jotoardhi ili wapate ujuzi wa kufanya kazi na Wajapan na kutuletea ujuzi huo hapa nchini”, alisema Njombe.
Kupitia ushirikiano huu unaoonyeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania, tuna imani kuwa nchi ya Japan itaendelea kuisadia Tanzania katika kuendeleza nishati ya jotoardhi kwakuwa ni nishati yenye tija katika kutimiza ndoto za Tanzania kwa kuifanya kuwa nchi yenye kipato cha kati kufikia mwaka 2020.
TGDC inatarajia kuanza kuainisha maeneo ya ushirikiano wa pande hizi mbili (TGDC na TOSHIBA) ikiwemo kuyawekea muda wa utekelezaji ambapo mwezi Machi mwakani, Wataalam toka TGDC wataweza kwenda nchini Japan kwa ajili ya kwenda kupata elimu zaidi kuhusu nishati hiyo.
Mtaalamu Mkuu toka Kampuni ya TOSHIBA Bwana Kentaro Kurahara anaeleza kuwa kampuni yao iko tayari kuisaidia Tanzania katika masuala yanayohusu jotoardhi na iko tayari kuomba ufadhili kupitia Serikali ya Japan ikiwemo kuwapa Wataalam wa TGDC elimu ya kutosha inayohusu nishati hiyo ili waweze kuhakikisha kuwa nishati hiyo inapatikana na kuleta maendeleo kwa Tanzania.
“Tunafuraha ya kushirikiana na TGDC katika kufanya tafiti zinazohusu jotoardhi kama mkataba wetu tuliousaini unavyosema, kupitia Serikali ya Japan na Shirika la JICA tutaomba ufadhili kwa ajili ya TGDC ili muweze kuleta wataalam wenu kuja kujifunza Japan pamoja kuwasaidia katika masuala mengine yanayohusu shughuli ya utafutaji wa nishati hii”, alisema Kurahara.
TGDC ikiwa kama Shirika Tanzu lililopo chini ya Kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limepewa lengo na Serikali la kuharakisha upatikanaji wa nishati ya jotoardhi kufikia Megawati 200 mwaka 2020. Kampuni hiyo imesajiliwa Disemba 19, 2013 na kuanza kufanya kazi Julai 2014 huku ikipewa jukumu la kuharakisha uendelezaji wa nishati ya Jotoardhi nchini ambapo mpaka hivi sasa TGDC imegundua Zaidi ya maeneo yenye viashiria vya jotoardhi ambayo yamegawanyika katika Kanda Nne ambazo ni Kanda kaskazini–Ziwa Manyara, Kreta ya Ngorongoro, Natron na Majimoto Mara, Kanda ya Mashariki–Utete (Pwani), Kisaki (Morogoro), Luhoi (Pwani), Kanda ya Magharibi–Ibadakuli (Shinyanga), Mtagata(Kagera), maeneo mengine ni Dodoma, Singida pamoja na Tanga.

Aibu ni chaguzi za Zanzibar, sio wapinzani kususa Bunge

BAADA ya yaliyotokea wiki iliyopita katika shughuli ya uzinduzi wa Bunge, watu wengi, hususan wanasiasa walio upande wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM0, wameita kitendo cha wabunge wa vyama vya upinzani kususia kusikiliza hotuba ya Rais Dk. John Magufuli ya uzinduzi wa Bunge kuwa ni kitendo aibu.

Wabunge-wa-UKAWA-wakitoka-bungeni-
Wabunge-wa-UKAWA-wakitoka-bungeni-Njonjo Mfaume

Uamuzi wa kugomea shughuli hiyo ulitokana na uwepo wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ambaye wapinzani wanadai hastahili kuendelea kuongoza Zanzibar. Wapinzani walitaka rais wao halali, Seif Sharrif Hamad, ndiye awepo.

Mmoja wa walioelezea fujo iliyotokea na kitendo cha mgomo wa wapinzani kuwa ni cha aibu ni Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai, huku Rais Magufuli mwenyewe akiita kitendo hicho kuwa ni cha kitoto.

Mimi nakataa. Sioni kuwa kitendo kile cha wapinzani ni cha aibu wala cha kitoto. Kuna vitendo vya aibu vimefanyika nchi hii ambavyo ndio hasa vimetufedhehesha mbele ya wageni.

Kwa mfano, nchi imeingia katika aibu kwa vitendo vya hujuma dhidi ya demokrasia ambavyo vimekuwa vikitokea kila mwaka wa uchaguzi kule Zanzibar na kuingiza nchi katika migogoro ya kisiasa.

Kutokana na migogoro hii ya kisiasa ya Zanzibar watu wamekufa na wengine kupata ulemavu katika 20 iliyoita. Tanzania imetoa wakimbizi wa kisiasa kwenda Kenya na sehemu nyingine duniani. Jumuiya ya Kimataifa, hususan Commonwealth imekuja kujaribu kutupatanisha wakati sisi ndio tegemeo la majirani zetu la kupatanisha wanapogombana. Na haya ndio mambo ya aibu.

Kuanzia uchaguzi wa 1995 ambao ni wa kwanza kufanyika baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hadi huu wa mwaka 2015 hakujawahi kuwa na uchaguzi uliopita bila kuzalisha migogoro mikubwa Zanzibar.

Uchaguzi wa mwaka 1995 ambao CCM ilitangazwa kuwa mshindi ulizaa mgogoro baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kudai kuwa imeporwa ushindi na kugoma kumtambua rais aliyetangazwa. Taarifa za waangalizi wengi wa kimataifa zilieleza masikitiko yao kutokana na vitisho dhidi ya raia na udanganyifu katika kuhesabu kura, jambo ambalo waliamini huenda lilipelekea matokeo yaliyotangazwa kuwa sio sahihi. Baadhi ya nchi wafadhili kama Norway na Sweden zilisimamisha misaada kwa Zanzibar kutokana na kadhia ile na hii kwa mtazamo wangu ndio aibu.

Kutokana na mgogoro huo, Jumuiya ya Madola ilisimamia mazungumzo ya upatanishi na hatimaye kufikiwa makubaliano yaliyosainiwa Aprili 29, 1999. Yalikuwa ni makubaliano mazuri ambayo yangetekelezwa huenda migogoro isingejirudia tena. Moja kati ya vipengele vya makubalino kuwa zichukuliwe hatua za kuhakikisha kuwa chaguzi za miaka ijayo ziwe wazi, huru, za kuaminika na zisiwe na mizengwe.

Hata hivyo, uzuri wa makubaliano ni kitu kingine, na dhamira ya kisiasa ya kutekeleza makubaliano hayo, hususan kwa upande wa watawala, ni jambo jingine.

Ni wazi kuwa makubaliano yale ambayo yalilenga katika kujenga misingi ya kuimarisha demokrasia, utawala bora na utengamano hayakutekelezwa kwani mwaka 2000 kulitokea mgogoro mwingine ambao ulizalisha wakimbizi waliokimbilia Shimoni, Mombasa huko Kenya. Na hii nayo ni aibu nyingine.

Pia, kufuatia uchaguzi wa mwaka 2000, mnamo Januari 27, 2001, watu 31 waliuwawa, 48, walipata vilema vya maisha na 243 walijeruhiwa, baada ya polisi kutumia nguvu kuzuia maandamano ya kupinga matokeo ya au uchaguzi Unguja na Pemba. Hii pia ni aibu iliyotufedhehesha kama taifa. Wengi wa wahanga hao walitoka kisiwani Pemba.

Chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa mwaka 2000 ilikuwa ni kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi na kuamuliwa kurudiwa katika majimbo kadhaa ambapo CUF haikukubaliana na uamuzi huo na kuamua kususia uchaguzi wa marudio. Katika uchaguzi huo wa marudio, CCM walijishindia kirahisi.

Mgogoro ukaendelea tena hata katika uchaguzi wa 2005, ambapo kwa mara nyingine tena, CUF waligoma kuitambua serikali ya Rais Amani Abeid Karume. Kutokana na kutoridhika kwa uwepo wa hali hiyo ya migogoro iliyogawanya jamii ya Wazanzibar, baadhi ya wanasiasa kutoka CUF na CCM walifanya jitihada ya kuanzisha mazungumzo ya kutafuta muafaka ambayo ndio yaliyozaa mpango wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010 ambayo ilikubaliwa na Wazanzibar wengi.

Mazungumzo yaliyozaa muafaka na ambayo yalifanywa na Wazanzibar wenyewe yalianza Machi 2009 na kufikia tamati Novemba 2009 kwa mkutano wa Rais Karume na Maalim Seif Sharif Hamad na kukubaliana kufuta tofauti za kisiasa zilizoigawa jamii ya Wazanzibari kwa zaidi ya miaka 15. Labda ni kutokana na muafaka wa kisiasa uliofikiwa uchaguzi wa mwaka 2010 haukuhijiwa sana, ingawa bado kulikuwa na figisu figisu nyingi.

Hata hivyo, mwaka 2015 umekuwa ndio kilele cha migogoro yote baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kuamua peke yake kufuta matokeo ya uchaguzi wote, ingawa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania, (NEC) haikufanya hivyo kwa matokeo ya Zanzibar. Inasemekana Jecha alitangaza uamuzi ule wa kufuta matokeo kwa kushinikizwa.

Jambo la kuzingatia ni kuwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Zanzibar mwaka huu waangalizi wote wameuita huru na wa haki, huku CCM wakilalamika kuibiwa. Kitendo cha CCM kimetajwa kuwa ni sawa kutia mpira kwapani katika mechi ya soka, baada ya kuona unaelekea kushindwa! Nikimjibu Magufuli, walichofanya CCM Zanzibar si sahihi.

Kuna hoja nyingi za kitaalamu zinazotolewa kuhalalisha yaliyofanyika Zanzibar, lakini yote hayo ni katika jitihada za kuficha aibu kubwa kabisa kuliko zote. Aibu kubwa kuliko zote ni kuwa kuna maana mpya ya demokrasia imetoholewa kule Zanzibar. Demokrasia Zanzibar maana yake ni ushindi kwa CCM, na si vinginevyo.

Najua kuna sababu za baadhi ya Wazanzibar na hata wanasiasa wa Tanzania Bara kuamua kutumia maana hii mpya ya demokrasia iliyotoholewa. Kule Zanzibar, CCM wanasema walipindua na hivyo basi hawako tayari kutoa serikali kwa vipande vya karatasi. Pia wanasema wana wasiwasi CUF watarudisha Waarabu. Huku Bara tunaogopa Uislamu wa siasa kali, kama ambavyo video maarufu ya William Lukuvi akizungumza kanisani ilivyotudhihirishia.

Mimi sio mtaalamu wa yote mawili. Sijui undani wa siasa za kimatabaka za Uarabu dhidi ya Weusi, Zanzibar. Kadhalika pia sijui ajenda halisi za CUF na uhusiano wake na siasa kali za Kiislamu, ingawa nimewahi kusoma makala ya Abdulrahman Kinana katika jarida moja huko nje akigusa suala la ugaidi.

Hata hivyo, kwamba hatusemi yaliyo vifuani mwetu kwa uwazi na badala yake tunatekeleza demokrasia ya hila na ghilba ni aibu kubwa. Tunamhofia nani kusema na kutenda kile tunachoamini? Nashauri CCM waifute CUF Zanzibar ili watawale peke yao badala ya kuendelea kuulea uhizbu na siasa kali za CUF kisa wanataka kuonekana na wao ni waumini wa demokrasia. Mimi sielewi kwa nini tunashindana katika uchaguzi kama kushindwa si matokeo ambayo tutakubali hata siku moja?

Baada ya hayo niseme kuwa kitendo cha wapinzani kususia bunge sio cha aibu. Ni kitendo kizuri cha kishujaa kuiambia dunia kuwa mambo si shwari Zanzibar. Nitamshangaa balozi wa nchi ya kigeni ambaye atashangaa kitendo kile kwa kiasi cha mshangao chini ya alioupata kwa yaliyotokea Zanzibar. Sana sana wengi watatupa uzoefu wa vituko vikubwa zaidi vilivyowahi kutokea katika mabunge ya nchi zao.

CHANZO: RAIA MWEMA

MKUU WA MAJESHI MSTAAFU, JENERALI GEORGE WAITARA AONGOZA TIMU YA MAAFISA 24 WA JESHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza katia hafla fupi ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa maofisa 24 wa jeshi la wananchi Tanzania .kulia ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara na kushoto ni Mnadhimu mkuu wa Jeshi la wananchi ,Luteni Jenerali ,Samweli Ndomba. 
Baadhi ya washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro. 
Mkuu wa majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara akizungumza katika hafla hiyo. 
Baadhi ya wapandaji. 
Mhifadhi Mkuu ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,( KINAPA) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki. 
Afisa Masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi akieleza jambo wakati wa hafala hiyo. 
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii,Balozi Charles Sanga ni mingoni mwa washiriki wa zoezi hilo la kupanda mlima Kilimanjaro. 
Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Lufunguro akiongozana na mgeni rasmi kwa ajili ya kukabidhi bendera kwa wapandaji mlima hao. 
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi,Fulgence Mponji akikabidhi bendera kwa Mkuu wa majeshi mstaafu ,Jenerali George Waitara ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo. 
Washiriki wakijiandaa kuanza safari. 
Safari ya kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro ikaanza kwa maafisa 24 wa JWTZ .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kada ya Kaskazini.

Rungu la TRA Yalishukia BAKWATA...Magari 82 Yaingizwa Kwa Jina lao Bila Kulipiwa Kodi..Watwaga Barua Nzito,


MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU)

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Pius Msekwa akitunuku Shahada ,Stashahada na Astashahada kwa wahitimu wa Chuo hicho wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Wahitimu wa kozi mbalimbali waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi,(MoCU) 
Miongoni mwa wageni waalikwa alikuwepo pia Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael. 
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Profesa Faustine Bee akizungumza wakati wa sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo hicho. 
Miongoni mwa wahitimu walikuwepo pia Mbunge wa viti maalum,Sharry Raymond pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Shaibu Ndemanga. 
Baadhi ya wakufunzi katika chuo hicho. 
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa (Kulia) akiteta jambo na Meneja wa benki ya NMB ,tawi la Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kashusho wakatiwa mahafali ya kwanza katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Kaimu Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha) Ndayizera Manta (Kushoto) akiwa na Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Profesa Gerald Monera wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Muongozaji wa sherehe ya mahafali hayo Cyril Komba akitoa muongozo wa shughuli hiyo iliyofanyika viwanja ya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi. 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Pius Msekwa akitoka katika viwanja vya Ushirika mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya mahafali ya kwanza ya chuo hicho. 
Baadhi ya wakufunzi wa Chuo hicho,Profesa Wakuru Magigi (kulia ) wakiwa na Mkuu wa Shule ya Polisi zamani Chuo cha Polisi Moshi,Matanga Mbushi . 
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi (kushoto) akiwa na mmmoja wa wakufunzi katika chuo hicho Dkt Kaleshu ,wakipozi katika picha ya pamoja na Mbunge wa Viti maalum CCM ,Sharry Raymond.
Picha zaote na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini (0755659929). 

PPF YAIBUKA KIDEDE KATIKA UTUNZAJI BORA WA HESABU ZAKE, YATWAA TUZO YA WA HESABU UPANDE WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII



Na K-Vis Media/Khalfan Said.
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.

Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. 
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Bw. Khamisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa kuwasilisha taarifa sahihi za hesabu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari, (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka 2014 kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano cha Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la Dar es Salaam, Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA
Bw. Mamri (wapili kulia), akigongesha glasi na mmoja wa waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wawakilishi wa PPF katika hafla hiyo.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top