Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MHE. BALOZI WILSON M. MASILINGI AKUTANA NA BI. CATHY BYRNE, MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA, IKULU YA MAREKANI (WHITE HOUSE) TAREHE 30 NOVEMBA 2015

Mhe. Balozi Masilingi (kulia) ametembelea ofisi ya Bi. Cathy Byrne, Mkurugenzi Mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Ikulu ya Marekani (White House). Katika maongezI yao, Bi. Cathy Byrne alimueleza Mhe. Balozi Masilingi jinsi Serikali ya Marekani inavyoridhishwa na mahusiano mazuri baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani. Pia alieleza kuhusu serikali ya Marekani kuridhishwa na hatua za serikali ya Tanzania, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
 Mhe. Balozi Masilingi amemhakikishia mwenyeji wake kuwa ataendeleza mashirikiano mazuri sana yaliyopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa njia ya diplomasia ya uchumi yenye lengo la kuhamasisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania.

==============================
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la Nchi za Afrika. 
Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Shabaha ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. 
Mhe. Balozi Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. 
Aidha aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia. 
Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki. Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P. Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania. 
 Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza program za maendeleo na huduma za serikali. 
 Bw. Larose, alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top