Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majliwa akizungumza na Waziri Mkuu
Mstaafu, Mizengo Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini
Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi ,
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akipokea taarifa ya
makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu,
Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam
Novemba 30, 2015.
Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu,
Mizengo Pinda wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt
Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi
Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Novemba 30, 2015.
Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza kabla ya
kukabidhi Ofisi kwa Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kwenye
ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya
kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu,
Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Novemba 30, 2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Maka Kikula.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya
kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu,
Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Novemba 30, 215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri
Mkuu Maka Kikula.
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akifurahia katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo
Pinda na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada
ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri kwa Waziri
Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
Novemba 30, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
--
WAZIRI MKUU mstaafu Mizengo Pinda
amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kumtaka aimarishe
ufuatiliaji wa maelekezo anayoyatoa kwenda ngazi za chini.
Akizungumza wakati wa makabidhiano
yaliyofanyika jana jioni (Jumatatu, Novemba 30, 2015), kwenye ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Bw.
Pinda alisema katika kipindi cha uongozi wake kulikuwa na ucheleweshaji
wa kupata majibu kutoka ngazi ya chini katika maelekezo aliyokuwa
akitoa.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na
ina mambo mengi ya kufuatilia. Kama kuna changamoto nilikumbana nayo ni
ucheleweshaji wa majibu kutokana na maagizo niliyokuwa nikitoa. Itabidi
uwe makini sana katika kufuatilia hili,” alisema Waziri Mkuu mstaafu.
Alimtaka ahakikishe kila idara
inakuwa na mpango kazi na kunakuwa na ufuatiliaji wa kila kilichopangwa.
“Pia ninashauri uandaliwe kikao na watu wa Hazina ili wakueleze jinsi
bajeti ya Serikali inavyoandaliwa ili iwe rahisi kwako kufuatilia
vipengele kadhaa vya bajeti ya Serikali pindi maswali yanapoulizwa
bungeni,” alisema.
Pia alimkabidhi taarifa yenye
kurasa 104 ambayo inaelezea majukumu mbalimbali ya taasisi na idara
zilizo chini ya Ofisi wa Waziri Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina taasisi
nane, idara nane na vitengo saba. Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya
Siasa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Kuratibu na Kudhibiti
UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao
Makuu (CDA). Nyingine ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC).
Idara zilizopo kwenye ofisi hiyo
ni Utawala na Rasimali watu, Sera na Mipango, Uratibu wa Maadhimisho ya
Kitaifa na Sekta binafsi na Uwezeshaji. Nyingine ni Bunge na Siasa,
uatibu wa shughuli za Serikali, Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Ofisi
Binafsi ya Waziri Mkuu.
Alisema pia ameridhishwa na kasi
ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu
wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi wao na uadilifu wao,
anaamini wataweza kuivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati
ambako Serikali imejielekeza kufika.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alimshukuru Waziri Mkuu mstaafu na kumuahidi kutekeleza
yote yaliyomo kwenye taarifa aliyomkabidhi. Pia aliahidi kusimamia kwa
karibu suala la ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa pamoja na yale
yanayotoka ngazi za juu.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na
Katibu Mkuu, Dk. Florens Turuka, Naibu Katibu Mkuu (OWM), Bibi Regina
Kikuli, wakuu wa taasisi zote nane, wakuu wa idara na vitengo vya Ofisi
ya Waziri Mkuu pamoja na Wasaidizi wa Waziri Mkuu walioko ofisi yake
binafsi.
Post a Comment