Mchezaji wa Liverpool Raheem sterling kinda ambae ameonyesha kiwango kikubwa msimu huu toka uanze akiwa namiaka 17 akipongezwa na Suarez baada ya kutoa pasi iliyomuwezesha kufunga bao wakati walipo pambana na Wigan katika mehi waliyoshinda goli tatu bila dhidi ya wigan
Raheem Sterling mwenye jezi namba 7 akijaribu kuwatoka wachezaji wa Sweden hiyo ikiwa ni mehi yake ya kwanza kuheza akiwa na Timu ya Uingereza.
Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amevionya vilabu vinavyo mnyemelea mchezaji kinda Raheem Sterling kuwa viachane na mawazo kwani mhezaji huyo hauzwi amesema hayo pamoja na kuwa mhezaji huyo hajasaini mkataba mmpya wa muda mrefu katika klabu hiyo.
Rogers anatazamia mchezaji huyo mwenye miaka 17 ambae wiki iliyopita aliichezea Uingereza dhidi ya Sweden katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kusaini mkataba wa muda mrefu katika klabu hiyo ya Liverpool baada ya mchezaji huyo kuonyesha kiwango kizuri mwishoni mwa wiki kwa kutoa pasi za mabao mawili kati ya matatu waliyopata dhidi ya Wigan.
Chanzo:Vyombo vya habari vya kimataifa.
Post a Comment