Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Swali la nyongeza la Mh.Zitto Kabwe laleta chereko Bungeni Hii imetokea muda huu Bungeni



Mh.Zitto Kabwe aliuliza swali dogo la nyongeza ''kuwa toka tupate uhuru hajawahi sikia Mkuu wa Majeshi(JWTZ) akitoka upande wa pili wa Muungano Je ni kwanini ?

Waziri wa Ulinzi akamjibu '' kuwa hilo ni suala la wakati kwani hivi sasa kuna majenerali wanne wako makao makuu huenda huko mbele mmojawapo akapata bahati hiyo.

Lakini akaaamsha chereko na makofi kwa wabunge pale aliposema kuwa hata yeye anajiuliza lini ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti wa chama atatoka Kigoma ?

Baada ya hapo kama kawaida ikawa ni kugonga meza kwa furaha na vigelegele Bungeni
hali iliyomfanya Mwenyekiti anaeongoza kikao asbuhi hii kuingilia kati.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

7 comments

sidhani km ni busara kujibu swali kwa swali na yy angeuliza swali lake la nyongeza km zitto alivyofanya hii nchi sijui inaelekea wapi?

Reply

Wajibu mwaswali hawanaga hoja zaidi ya kuwaza mambo ya kitoto,sasa CDM ina miaka 50?

Reply

jamani hayo ndo mambo ya siasa

Reply

Mh. Zitto hapo unamaanisha nini? uwenyekiti wa CDM au? Maslahi ya watanzania mbele uongozi si muhimu kamanda! Hata kama ni mfano haufai maana tutashindwa kukuelewa!

Reply

Mimi binafsi naiheshimu sana Chadema na hoja zake.Lakini swali hili la nyongeza la Zitto ni la aibu kwa CDM na si swali la kistaarabu na utu uzima.Tanzania tunapaswa kumpa kazi mtu ya Uongozi kwa sifa zake na si ukanda, ukabila na Udini.Haya ni yale yale amboya watu wengine wanataka taasisi za serikali zianze kuajili kwa uwiano wa kidini.Huu ni uchochezi Zitto tunaomba utuombe radhi mashabiki, wapenzi na wanachama wa CDM

Reply

mh.Zitto kwa hili hapana,utaturudisha kulekule kwenye uzanzibari na uzanzibara.ifike
hatua tuangalie uwezo wa mtu kama anatufaa basi tumtumie,atufikishe pale tunapotaka watanzania tulio wengi na si kuangalia mzanzibari au mzanzibara.Maana naogopa tusije tukafikia hadi kwenye kuangalia dini/zamu ya mtu katika kuwaongoza watanzania
na si uwezo wake.

Reply

Yale yalee, Tz siku zote ukizungumzia kuwepo usawa wa fursa katika nyanya mbali mbali, huo ndio utaitwa ubaguzi wa kila kitu kimajimbo, kidini na kila ujuacho kama ubaguzi. Visingizio viiingi mtavunja amani, sijui mtabagua watanzania. Kama hali tunayoenda nayo hakuna usawa au anaefinywa akisema mnaniumiza au mwengine akimsemea ndio ndio mbaguzi ?

Mh Zitto suala lako ni sawa wahemiwa watoe jawabu si utani. Hayo ya uwezo sijui umajimbo, udini ndiyo yaliyotufikisha hapo Mh anapouliza. Tuyaondoeni

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top