Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akisalimiana na Wananchi na
wanachama wa chama hicho waliofika kumpokea katika Viwanja vya CCM
Kisiwandui Mjini Zanzibar jana,akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu wa
Halmashauri ya CCM na Uchaguzi wa Viongozi wa juu katika chama
hicho.
Picha na Ikulu ya Zanzibar
Kwa ufupi
WAGOMBEA WAITUMIA KAMA KETE YAO, MWIGULU APEWA SIFA KUIKABILI, RAIS KIKWETE ATAKA KUKABILI UPINZANI KWA HOJA
..............
Jina la Chadema lilianza kutawala katika mkutano
huo, Jumapili Novemba 11 mwaka huu, wakati makada wa chama hicho
waliokuwa wakigombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec), wakijinadi kwa
wajumbe.
Chadema ilitumiwa na baadhi ya wagombea wa nafasi 10 za Bara na Visiwani kama kete yao ya kuchaguliwa kupata nafasi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na
Uratibu), Stephen Wassira wakati akiomba kura aliwaambia wajumbe wa
mkutano huo wampe kura ili apeleke kilio Chadema.
Alisema akichaguliwa mjumbe wa Nec atapata nguvu ya kupambana na Chadema.
Alisema akichaguliwa mjumbe wa Nec atapata nguvu ya kupambana na Chadema.
“Nipeni kura ili nipate nafasi nipeleke kilio
Chadema,” alisema Wassira huku akishangiliwa wakati akiomba kura na Rais
Jakaya Kikwete akimwita kwa jina la utani ‘Tyson’.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, (UVCCM), Martine Shigela wakati akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano huo alisema yeye ndiye anayeongoza jeshi la ardhini linalopambana na wapinzani wanaopiga kelele.

“Mimi ndiye ninayeongoza jeshi la ardhini linalopambana na wapinzani wanaopiga kelele,” alisema.
Naye Mwanamanga Manguga aliwaomba wajumbe wampigie
kura ili CCM aipeleke Chuo Kikuu cha Dodoma anakosoma na kwamba, tayari
ameshaingia katika mapambano.
Alisema katika uchaguzi wa udiwani uliopita Kata ya Msalato mjini Dodoma, wafuasi wa Chadema walimpiga mawe na kumjeruhi wakati akitetea chama hicho.
Alisema katika uchaguzi wa udiwani uliopita Kata ya Msalato mjini Dodoma, wafuasi wa Chadema walimpiga mawe na kumjeruhi wakati akitetea chama hicho.
Chadema pia ilikuwa ikitamkwa sana na
mshereheshaji wa mkutano huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho
Nape Nnauye wakati akitoa matangazo mbalimbali kwa wajumbe.
“Watawezaaa… Wataweza hao Chadema…,” alisikika akiwaambia wajumbe wa
mkutano huo nao wakimjibu; “Hawaweziii!”
Vilevile, Chadema ilikuwa ikitajwa sana na wapambe
wa wagombea wa nafasi ya Nec ambao mara kwa mara walisikika wakiwaambia
wachague wagombea wao kwa sababu ndio wenye uwezo wa kupambana na
Chadema.
Mpambe mmoja wa mgombea mmoja ambaye hakupenda
kutajwa jina lake, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa chama hicho
kinapaswa kuchagua safu ya uongozi ambayo itakuwa ni mwiba kwa Chadema.
Hata Rais Jakaya Kikwete wakati akifunga mkutano
huo, Novemba 13 mwaka huu, aliwataka wanachama wa chama hicho kuwajibu
wapinzani kwa hoja, kama alivyofanya, aliyekuwa Katibu wa Uchumi na
Fedha wa chama hicho, Mwigulu Nchemba wakati wa Bunge la Bajeti mwaka
huu.
Alisema, “Baada ya wapinzani kutoa bajeti yao,
kijana wetu, Mwigulu alisimama akaivunjavunja bajeti yao. Wakanywea.
Ndivyo tunavyopaswa kufanya.
Mkijibu kwa hoja wanatulia, siyo Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.
Wakati wa Bunge la Bajeti, Mwigulu alipinga bajeti mbadala ya wapinzani akisema imeandaliwa na watu wasiojua uchumi na kudhihirisha kuwa alikuwa akiiponda aliamua kuitupa nakala ya bajeti hiyo bungeni.

Kitendo hicho kilishangiliwa sana na wabunge wa CCM waliokuwa bungeni huku baadhi ya wabunge wa upinzani wakipinga.
Vilevile, katika mkutano huo mkuu wa CCM, jina la
Chadema lilionekana katika fulana zilizovaliwa na baadhi ya wanaCCM
ambazo zilikuwa na maneno “Vua Gwanda, Magamba, Vaa Uzalendo.”
Sare maalumu za Chadema zinazovaliwa na makada na viongozi wa chama hicho, zinajulikana kama Magwanda.
Magamba ni neno ambalo lilitokana na uamuzi wa
chama hicho kutaka kufanya mabadiliko ndani ya CCM kwa kujisafisha
uliotangazwa na Mwenyekiti wake chama hicho “kujivua gamba”.
Baada ya hapo, watu ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi na kukipaka matope chama hicho wakaanza kuitwa magamba ndani ya chama hicho.
Hivyo, ujumbe huo uliokuwa katika fulana hizo
ulikuwa ukiwaambia wananchi kuachana na Chadema pamoja na watu wasiokuwa
wasafi ndani ya chama hicho kikongwe nchini.
Chadema imeanzisha Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo inafanyika kwa kufanya mikutano nchi nzima, ambayo imekuwa na athari kubwa kwa CCM.
Moja ya athari hiyo ni pamoja na kuzoa wanachama na viongozi ambao wanajiunga na chama hicho na kujiongezea umaarufu.Chadema imeanzisha Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo inafanyika kwa kufanya mikutano nchi nzima, ambayo imekuwa na athari kubwa kwa CCM.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Post a Comment