Golikipa
wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga
wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya
penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka
dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao
wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini
Mwanza.

Wachezaji
wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete
kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Mchezaji
wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu
ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi
kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na
hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji
wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu
ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baadhi
ya mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kununu
tiketi na kujionea kandanda safi kabisa kati ya timu ya Yanga na Black
Leopards ya Afrika kusini.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu
ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga
imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini
Mwanza.
Mtanange ukikaribia kuanza.
Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa
ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete
akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa
kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
Nginja nginja tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya Yanga.
Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.
Picha na JICHIE BLOG-jijini Mwanza.

















Post a Comment