Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA:HOROHORO MPAKANI TANZANIA NA KENYA

 Mpaka kati ya Tanzania na Kenya upande wa Mkoa wa Tanga Horohoro ukionyesha geti la kuingilia kwa Upande wa Tanzania kuelekea Kenya ambapo magari na watembea kwa miguu wakivuka kuingia na kutoka.
 Gari za abiria kutoka Tanga mjini kuwaleta watu boda la Horohoro zikiwa zimepaki kusubiri abiria tayari kwa kuelekea Tanga mjini.Usafiri upo muda wote kwa mujibu ya wenyeji kila baada ya nusu saa gari inaondoka iwe na abiria au haina lazima ielekee mjini Tanga hivyo kuwarahisishia wenyeji nawageni wafikao eneo hilo.
 Boda boda hawakosekani kila eneo wapo pia Horohoro wakichapa kazi.Zipo zenye usajilii wa Kenya na wengine wa Tanzania japo sio wengi.Gari zilizosheheni mizigo zikiwa kwenye foleni tayri kwa kukaguliwa kabla ya kungia Tanzania.Eneo hili lipo katikati ya Kenya naTanzania ambapo unaruhusiwa kuingia na kutoka.

 Ukifika eneo hili unakutana na boda ya Kenya ambapo kuvuka hapa kwa wewe uliyetoka Tanzania lazima uwe na umefuata taratibu zote za uhamiaji.Watembea kwa miguu haoni Wakenya ambao huwa wanavuka upande huu wa pili kuelekea boda yaTanzania ambayo huruhusiwa kwa yeyote kuja kutembea nakurudi upande wake.

 Majengo mapya yamekuwa yakijengwa eneo hilo kama taswira inavyoonekana ambapo tulielezwa ni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 Katika kuimarisha mpaka na shughuli mbalimbali ukarabati nao unashika kasi hapo ni upande wa Kenya wakiendelea na ujenzi
Magari ya mizigo yanaonekana yakiwa kwenye foleni kuingia/kuvuka boda ya Tanzania.

Picha na Rundugai Blog Team.

Mpaka kati ya Tanzania na Kenya ukitokea Tanga mjni unaitwa Horohoro na unaunganishwa kwa Barabara ya Lami kutoka mjini Tanga hivyo usafiri wake ni wa uhakika na halichukui muda mrefu hivyo kukuwezesha kwenda horohoro na kurudi mjini Tanga bila wasiwasi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top