Je wajua kuwa sasa unaweza ingia Sauzi bila kuwa na Visa?
Yes ni kweli kabisa unaweza ingia Sauzi bila kuomba visa. Unachotakiwa tuu ni
kuwa na Passport yako ya Tanzania, hapa nazungumzia Passport ya kimataifa kama
hiyo pichani hapo juu.
Bila shaka unafahamu kuwa kwa nchi za Afrika mashariki si
lazima uwe na hiyo Passport ya kimataifa, kuna Passport maalum za Afrika
Mashariki. Ila leo tuzungumzie namna ya kupata hiyo Passport ya kimataifa.
Bei:
Kwa mujibu wa website ya uhamiaji immigration.go.tz, ni
kuwa utahitaji kulipia Tshs. Elfu Hamsini. Malipo haya yanalipwa hivi: Elfu
KUMI wakati wa kuchukua fomu, halafu ukirudisha fomu unalipia ElFU AROBAINI.
Masharti :
Inakupasa uwe na cheti cha kuzaliwa, na pia uwe
na cheti cha kuzaliwa cha mmoja wapo wa mzazi wako. Kama mzazi hana cheti basi
atahitaji kupata kiapo cha mahakamani kuthibitisha kuwa ni mtanzania. Kiapo
hicho huitwa Affidavit.
Pia unahitaji kuwa na picha TANO za kiwango maalum cha Passport
size, maelezo ya namna ya kupiga picha hizi zinazohitaji utayapata kwa ofisi ya
uhamiaji utakayoenda kuomba Passport. Ushauri kwako, usijipigie tuu picha
ukaziwasilisha uhamiaji, hakikisha unawasiliana na ofisi ya uhamiaji nao
watakupa maelekezo sahihi kuhusu picha wanazotaka.
Fomu ya maombi:
Utatakiwa uende ofisi ya uhamiaji na kulipia fomu maalum ya maombi. Wewe
utajaza hiyo fomu ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa na sehemu maalum ya mdhamini
wako kujaza na kutia saini. Wewe utatakiwa kutia saini mbele ya ofisa wa
uhamiaji siku ya kuirudisha fomu husika.
Mahitaji mengine:
Utahitajika kuwa na sababu maalum ya
kwanini unataka kusafiri kwenda nje ya nchi. Uthibitisho maalum unahitajika,
mfano barua ya mwaliko wa kumtembelea mtu aliyepo nje ya nchi, au barua ya
kuitwa kufanya kazi nje ya nchi, au barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo nje ya
nchi, uthibitisho wa tiketi ya kurudi toka nchi unayotaka kutembelea
kibiashara, au uthibitisho mwingine kama wa safari ya matibabu, au michezo.
Inachuku muda mpaka kupata Passport?:
Inategemea, ila kwa
kawaida si zaidi ya wiki mbili toka uwasilishe fomu kamili na kutimiza masharti
yote.
1 comments:
Natakiwa kuonesha bank statement kwa afisa uhamiaji?
ReplyPost a Comment