Baada ya kuichapa timua ya Azam FC kwa bao 1-0 mwishoni mwa wiki,
timu ya Young Africans Sports Club leo imeingia kambini katika Hoteli ya
Tansoma katikati ya jiji kujiaandaa na mechi inayofuata dhidi ya timu
ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumatano katika dimba la
Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Young Africans ambayo iliwapa furaha washabiki, wapenzi
wa soka na wanachama wake kwa soka safi la ufundi wa hali ya juu,
itashuka dimbani kuwakabili wakata miwa hao ambao katika mchezo wa awal
waliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika katika dimba la
Kaitaba mjini Bukoba.
Young Africans yenye jumla
ya point 39 na mabao 34 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa itashuka
dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo
huo ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya VPL na hatimaye iweze
kutwaa Ubingwa huo.
Mara baada ya mazoezi ya leo
asubuhi, kocha mkuu Brandts amesema anashukuru vijana wake kwa kufanya
kile alichowaagiza, nidhamu ya hali ya juu na kushika maelekezo yake
ndio vitu vilivyopelekea kuendelea kuibuka na ushindi katika michezo
mbali mbali waliyocheza.
Nawapongeza washabiki,
wanachama na wapenzi wa Yanga waliojitokeza kwa wingi siku ya jumamosi,
kuja kuwashangilia vijana, kikubwa nawaomba waendelee na moyo huo huou
kwani waliwapa nguvu vijana na kuwafanya wacheze kwa kujiamini mda wote
wa mchezo 'alisema Brandts'.
Aidha Brandts alisema
matokeo ya juzi yameendelea kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya
kuelekea kutwaa Ubingwa na atahakikisha wanajitahidi kushinda kila
mchezo ili kujiweka katika mazingia mazuri ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu
ya Vodacom.
Kikosi
cha wachezaji 26 na benchi la ufundi wote wameingia kambini katika
Hoteli ya Tansoma mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi na wachezaji wote
ni wazima kiafya na kiakili hivyo hakuna mcheaji hata mmoja ambaye ni
majeruhi.
CHANZO:YANGA
Post a Comment