1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri.
Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni
mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.
2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu
mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda
kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi
iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa
unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.
3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya
yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea
mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye
karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali
4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako
amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na
mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko
kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa
wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa
huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana
nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi
akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.
5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana
kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya
mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana
na kufahamiana zaidi.
6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda
kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia
kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini
7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara
mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani
au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia
unampenda.
8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa
sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka
pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.
9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda
ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla
hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana
huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda
kubembelezwa.
10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na
kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana
kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda
mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa
jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho
kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia
silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa
pia.
Post a Comment