Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KIGWANGALLA AIBUKA NA HOJA YA MUUNGANO

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk Hamisi Kigwangalla amesema ili kuondoa mvutano kuhusu muundo wa Muungano ni lazima yafanyike mambo mawili, ambayo ni kuongeza muda wa Rais kuwa madarakani au kubadili Katiba katika maeneo yanayohusu Tume ya Uchaguzi (NEC) pekee.
Akizungumza jijini jana, Dk Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Nzega (CCM) alisema mambo hayo mawili hayawezi kukwepeka kwasababu hata kama Katiba Mpya itapatikana, bado itahitajika kufanya mabadiliko ya sheria mbalimbali, zoezi ambalo alidai litachukua takriban miaka miwili.
“Namwomba Rais Jakaya Kikwete aingilie kati. Atumie mamlaka yake kusitisha mchakato wa Katiba mpaka itakapoundwa Tume nyingine ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la muundo wa Muungano,” alisema na kuongeza;
“Baada ya maoni hayo ipigwe kura maalumu kuhusu jambo hili ili Watanzania washiriki kikamilifu na upatikane uamuzi sahihi na unaokubalika na wengi. Si jambo la busara kujadili Rasimu ya Katiba bila kuwa na suluhu inayokubalika kuhusu muundo wa Muungano.”
Alisema kuwa kitendo cha Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba kupendekeza muundo wa Serikali tatu, utalivuruga Bunge la Katiba iwapo wataibuka wajumbe na kupinga muundo huo.
Alisema kuwa kama muundo wa Serikali tatu utapingwa, muundo wowote utakaopitishwa utasababisha kuwekwa vifungu vipya jambo ambalo litazidi kuleta mkanganyiko katika mchakato mzima wa Katiba.
“Ndiyo maana nikasema mchakato huu usitishwe kwa muda ili watu wote tukubaliane juu ya muundo wa muungano tunaoutaka. Wabunge wa Bunge la Katiba tukiukataa huu muundo wa Serikali tatu kipi kitatokea?”alihoji.
Dk Kigwangalla alisema Tume hiyo bado haijatoa majibu katika mambo kadhaa; njia ilizotumia kupendekeza Serikali tatu, kwa nini walipendekeza mfumo huo na nani atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Tanganyika.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo wakati tayari Rais Kikwete ameshateua wajumbe 201 wa Bunge hilo ambalo linaanza Februari 18 mjini Dodoma.
CHANZO:Mwananchi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

1 comments:

Huyo jamaan ni kichaaa nini

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top