Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KIGWANGALLA:ZAMA ZA WAZEE ZIMEKWISHA


Mbunge wa Nzega,Dk. Khamis Kigwangallah
 
 
Mtihani kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumteua mwanachama atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015 umezidi kuzua mapya, baada ya kada wake mmoja miongoni mwa waliokwishatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo kuponda wazee kwamba hawana tena nafasi ya kuongoza.
Kada huyo, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangallah, amesema wazee wakae pembeni kwa sababu zama zao zimekwisha  kwani safari hii ni zamu ya vijana kushika hatamu ya uongozi.

Msisitizo wa vijana kutaka kuwania nafasi ya urais mwakani ulitangazwa juzi na Dk. Kigwangallah  wakati akizungumza na vijana wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) jijini Mwanza.

Wakati Dk. Kingwangalah akizungumza na vijana hao naye Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alikuwa jijini hapa kushiriki hafla ya kuzindua albamu ya kwaya ya Philidephia Gospel iitwayo ‘Deni la dhambi ambaye naye aligusia masuala ya urais 2015.

Nchemba na Kigwangallah kwa nyakati tofauti waliwahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu 2015 kwa tiketi ya CCM.

Akizungumza na vijana wa chama hicho tawi la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) jijini Mwanza, Dk. Kigwangallah, alisema lazima vijana walazimishe mabadiliko kuanzia sasa na kuwaondoa wazee madarakani.

“Lazima vijana tubadilishe mabadiliko, wazee watatudharau lakini lazima waondoke ili kupisha kizazi cha dot.com…hawa wazee mtazamo wao ni wa kizamani hawajui kama kuna facebook, whatsap, instragram vitu ambavyo vijana wanatumia,” alisema Dk. Kigwangallah.

Alisema ameonyesha nia ya vijana kuchukua uongozi na maajabu yataonekana mwezi Mei mwakani katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM mjini Dodoma wa kuteua kada wake atakayepeperusha bendera ya mbio za urais.

Dk. Kigwangallah alisema vijana lazima waitetee nchi yao kutokana na kundi la watu wachache kuiba zaidi ya Sh.bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Banki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwamba vijana wa CCM kukaa kimya na kuliwapa nafasi wapinzani kuisimamia hoja hiyo.

“Mtu akiiba maslahi ya umma kisha anatumia kivyake hafai ndani ya chama chetu…kwanini vijana tukae kimya kuwaacha watu hawa, kinachotakiwa ni kuwashughulikia wote waliofanya ufisadi huo wa pesa za Escrow,” alisema.

Alisema hivi karibuni watu wenye heshima zao walionekana wanachukua fedha benki kwa kutumia mabegi makubwa na mifuko ya plastiki, wakati benki ni sehemu salama na sahihi kuhifadhi fedha.

“Vijana wa UVCCM tungewajibika kusimamia hili la Escrow na kuingia mitaani kulipinga, lazima akina Kafulila (David), Zitto Kabwe wangepotea na hoja yao…UVCCM ya Guninita (John) ni tofauti kabisa na hii ya sasa iliyojaa ushabiki wa viongozi, haikosoi serikali na kushabikia wagombea urais mafisadi,” alidai.

Naye Nchemba akizindua albamu ya kwaya ya Philidephia Gospel iitwayo ‘Deni la dhambi’ uwanja wa CCM Kirumba, alisema viongozi wanaochanganya waganga wa jadi na kanisa hawafai katika jamii.

Alisema ili kupata uongozi lazima umwamini mwenyezi Mungu kama yeye (Nchemba) alivyowahi kuombewa wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

“Uchaguzi ujao nitafanya hivyo, lakini wale viongozi wanaochanganya njia mbili za waganga na Mungu, hawafai bali wanatakiwa kumtegemea Mungu wakati wote,” alisema Nchemba.

Nchemba alichangisha zaidi ya Sh. milioni 10 katika uzinduzi huo wa albamu ya ‘Deni la Dhambi’.
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top