Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MPAMBANO WATANI WA JADI LIVE SUPER SPORT



Mechi tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza kati ya saa 1.30 jioni na saa 1 kamili usiku.Hii ikiwa ni fursa nyingine adhimu kwa Klabu zetu na wachezaji kujitangaza nchi za nje.

Pia kwa wachezaji wetu ni wakati wa kutia juhudi ili kuweza kufaidika na vipaji vyao kwani wataonekana vyema na mawakala mbalimbali wanao tafuta vipaji kwa ajili za Klabu za Ulaya au hata za hapa Afrika Mfano:Tp Mazembe au Afrika ya Kusini ambapo Ligi yake imekuwa ikitangazwa mno Duniani.

Tarehe 28 Septemba mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Mechi yaMabingwa watetezi  Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 11 kamili jioni.

Mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.

Mechi ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua vumbi saa 1 kamili usiku.Mpambano huu unatazamiwa kuvutia mamia ya mashabiki ukizingatia kipindi cha usajili kilivyokuwa na malumbano ya wakongwe hawa wawili wa Soka Tanzania Bara.

Kunyang'anyana kwa wachezaji miongoni mwa vilabu hivi viwili kunalifanya pambano hilo kusubiriwa kwa hamu na mashabiki hao ili kuona kama usajili waliofanya una tija kwa klabu zao au zilikuwa ni siasa za soka la bongo.

Huku Mashabiki wa Yanga wakitaka kulipiza kisasi cha kipigo walichopata toka kwa Simba katika mechi ya mwisho wa msimu uliopita cha bao 5-0 hali iliyopelekea kuchaguliwa kwa uongozi mpya mtaa Jangwani,ambao umeleta matumaini mapya kwa wanazi hao wa Yanga.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top