Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye inadaiwa ameshinikiza kurudishwa kwa
safu yake ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) lengo ikiwa ni
kukinusuru chama na Serikali yake.
Kwa ufupi
KUNA kila dalili kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amekirejesha chama hicho katika
mikono ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, baada ya kuwateua katika nafasi
za juu za CCM waliokuwa wasaidizi wa mtangulizi wake huyo.
KUNA kila dalili kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Rais Jakaya Kikwete amekirejesha chama hicho katika mikono ya Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa, baada ya kuwateua katika nafasi za juu za CCM
waliokuwa wasaidizi wa mtangulizi wake huyo.
Wasaidizi hao ni pamoja na Makamu Wenyeviti,
Philip Mangula (Tanzania Bara) na Dk Ali Mohamed Shein (Tanzania
Zanzibar) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, ambao
walichaguliwa na kuteuliwa katika vikao vya juu vya CCM vilivyomalizika
hivi karibuni mjini Dodoma.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa
wanasema kwamba lengo la mabadiliko yaliyofanywa ni kujaribu kurejesha
utaratibu wa CCM kuisimamia Serikali, utamaduni ambao ni kama ulikuwa
umekufa, tangu Serikali ya awamu ya nne ilipoingia madarakani.
Mhadhiri wa zamani wa Chuo cha Ushirika Moshi,
Akwiline Kinabo anasema kwamba kuna kila dalili kuwa Mkapa ana ushawishi
katika uteuzi wa safu mpya katika sekretarieti ya chama hicho.
“Inawezekana Mangula, Kinana na Dk Shein walifanya
vizuri sana enzi za Mkapa hadi akashawishi waingizwe kwenye
sekretarieti ya sasa, lakini enzi za Mkapa na sasa ni kama mlima na
kichuguu,” alisema.
Kinabo ambaye katika uchaguzi wa CCM uliomalizika
mwezi uliopita aligombea Nec kupitia Moshi Mjini na kushindwa, alisema
viongozi hao hawawezi kwenda na kasi ya siasa za vijana wa sasa.
Kada huyo wa CCM alihoji, ”Hivi Kinana au Mangula
wataweza kushindana na hoja za Halima Mdee na Zitto Kabwe majukwaani?
Kuna vijana wengi wameshinda Nec kwa nini wasiingizwe huko?”
Naye mwasisi wa CCM na kada wa siku nyingi wa
chama hicho, Steven Mashishanga alisema kuwa viongozi waliochaguliwa
waliwahi kufanya vizuri siku zilizopita, hivyo hakuna shaka kwamba
watarejesha utaratibu wa kutekeleza mwongozo wa chama wa 1981.
“Ukisoma mwongozo huo kuanzia ibara ya 81 utabaini
kwamba kazi ya chama ni kuisimamia Serikali, hili lilikuwa halifanyiki
kwa muda mrefu katika awamu ya nne, sasa hawa waliochaguliwa lazima
waturejeshe katika msingi huo,” alisema Mashishanga ambaye aliwahi kuwa
Mkuu wa Mikoa ya Mwanza, Tabora na Morogoro.
Hata hivyo, alisema wasiwasi wake ni iwapo uongozi
mpya utaweza kuleta mabadiliko kutokana na Halmashauri Kuu (NEC) ya
chama hicho kujaa wabunge na mawaziri ambao hawawezi kuwa na ujasiri wa
kuukosoa uongozi wa juu wa chama.
“Mimi kwangu msimamo unabaki kwamba chama ni chama na Serikali ni Serikali, huwezi kuwa chama na Serikali kwa wakati huohuo.
Sasa wewe jiulize, hivi waziri anaweza kukaa
kwenye NEC akamkosoa mwenyekiti ambaye ni Rais wake? Hapo kuna kasoro
ambayo tunapaswa kuirekebisha,” alisema Mashishanga.
Mangula, alikuwa Katibu Mkuu wa CCM takriban kwa miaka 10 ya
utawala wa Mkapa, huku Kinana ambaye akiwa amefanya kazi za chama kwa
muda mrefu awamu ya Mkapa.
Kwa upande wake Dk Shein aliibuliwa kuwa kiongozi
wa juu serikalini na Mkapa, wakati alipomteua kuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julai 13, 2001 kutokana na kifo cha
ghafla cha mtangulizi wake, Dk Omar Ali Juma kilichotokea Julai 4, mwaka
huo.
Philip Mangula
Mangula ambaye ametumikia nyadhifa mbalimbali za chama na Serikali kwa miaka mingi, aliteuliwa na Mkapa kuongoza chama hicho, kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2007.
Philip Mangula
Mangula ambaye ametumikia nyadhifa mbalimbali za chama na Serikali kwa miaka mingi, aliteuliwa na Mkapa kuongoza chama hicho, kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2007.
Katika uongozi wake, Mangula anasifika kwamba
alikijenga chama na kuwa imara na kwamba wakati wa utawala wake hapakuwa
na makundi yaliyotishia uhai wa CCM kama ambavyo imejitokeza kwa siku
za karibuni.
Mangula ambaye ni mmoja wa makada wakongwe ndani
ya CCM, mbali ya kuwa Katibu Mkuu, amewahi kuwa mwalimu wa Chuo cha
Chama Kivukoni kwa muda mrefu.
Pia amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,
Mkuu wa Mikoa ya Kagera, Tabora na Mwanza na baadaye kuingia katika
utendaji wa chama.
Hata hivyo, alipata pigo la kisiasa baada ya Rais
Kikwete kuingia madarakani alipounda safu mpya ya uongozi wa chama hicho
mwaka 2007 na kumwacha.
Mkongwe huyo wa siasa nchini, aliamua kurejea
nyumbani kwake Kijiji cha Imalinyi, Wilaya ya Njombe na kujikita katika
kilimo cha nyanya.
Mangula wakati akiwa katibu mkuu, ndiye
aliyesimamia mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na Rais Kikwete kufanikiwa kugombea.
Kinana na Dk Shein
Kwa upande wake, Kinana, alikuwa msimamizi mkuu wa kampeni za urais za Rais Mkapa wakati anaingia madarakani 1995 na baadaye akaongoza kampeni yake ya kuwania kuongoza ngwe ya pili 2000.
Kinana na Dk Shein
Kwa upande wake, Kinana, alikuwa msimamizi mkuu wa kampeni za urais za Rais Mkapa wakati anaingia madarakani 1995 na baadaye akaongoza kampeni yake ya kuwania kuongoza ngwe ya pili 2000.
Mbali ya kuongoza kampeni yake Rais Mkapa alikuwa
akimtumia Kinana katika mambo ya kisiasa mengi ikiwamo kumteua katika
Kamati Kuu ya chama kwa muda mrefu.
Uhusiano huo mkubwa wa Mkapa na Kinana ndiyo ambao
umemfanya Rais huyo mstaafu kuendelea kufanya naye kazi, kwani hivi
sasa ni mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation).
Kinana aliingia katika bodi hiyo inayoogozwa na
Meja Jenerali Mstaafu, Herman Lupogo mwishoni mwa mwaka jana. Baadhi ya
wajumbe wenzake katika bodi hiyo ni Dk Gilbert Mliga, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, Dk Yahya Ipuge, Eileen
Swain a Profesa Eden Maro.
Kwa upande wa Dk Shein wakati alipoteuliwa na
Mkapa hakuwa mtu ambaye alikuwa akifikiriwa katika nafasi ya Makamu wa
Rais, kwani hakuwa na jina kubwa miongoni mwa wanasiasa wa Zanzibar.
Rais Mkapa aliyaweka kando majina makubwa ambayo yalikuwa
yakitarajiwa wakati huo, hatua ambayo inamfanya Dk Shein kuikumbuka
Julai 13, 2001 kuwa siku ya pekee katika maisha yake.
Akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti wa CCM mjini Dodoma wiki iliyopita, Dk Shein alisema tarehe
13 ni siku maalumu katika maisha yake, kwani ndiyo siku alipoteuliwa
kushika wadhifa wa makamu wa rais, wakati huo akiwa hajui pa kuanzia.
“Leo hii ni tarehe 13, lakini si mwezi Julai bali
mwezi Novemba, nachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, lakini tofauti
na wakati ule, leo ninafahamu pahala pa kuanzia,” alisema Dk Shein.
Wasemavyo wanaCCM
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Wilaya ya Nzega, Hussein Bashe akizungumzia uteuzi huo alisema, ni mzuri kwa sababu umechanganya wazee na vijana.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Wilaya ya Nzega, Hussein Bashe akizungumzia uteuzi huo alisema, ni mzuri kwa sababu umechanganya wazee na vijana.
Alisema safu hiyo mpya ya chama inaonyesha taswira
ya mwelekeo wa chama, kwani uzoefu wa Mangula na Kinana ambao
wametumikia chama tangu enzi ya utawala wa Rais Mkapa utasaidia sana
kukifanya kiendelee kuongoza nchi hii.
Bashe alisema uteuzi wa safu hii ndiyo suluhisho la migogoro iliyopo ndani ya chama hicho.
“Migogoro na mpasuko ndani ya chama chetu sasa basi,” alisema.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja
alimpongeza Rais Kikwete kwa kuteua watu wanaofaa katika uongozi wa
chama hicho.
Alisema uzoefu wa muda mrefu wa Kinana na Mangula
ambao wametumikia hata awamu nyingine ya uongozi wa nchi, unatosha
kukifanya chama hicho kuwa na safu ya uongozi ambayo ni ya ushindi.
Mgeja alisema anaamini safu hiyo imefungua ukurasa
mpya wa matumaini katika chama hicho ambacho kilikuwa kimekumbwa na
migogoro mingi.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
Post a Comment