Hoyce Temu akimpa mkono wa pole mke wa Marehemu Daudi Mwangosi alipoitembelea familia hiyo kuifariji. Mwanaharakati
wa kijamii Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania
amefanya ziara mkoani Iringa na kupitia nyumbani kwa familia ya
mwandishi aliyeuawa Daudi Mwangosi na kuwajulia hali. Hoyce
Temu kwa pamoja na kundi zima la waandaaji wa kipindi cha mimi ni
Tanzania waliwasili katika nyumba ya mjane huyo Bi. Itika Mwangosi
kumsabahi na kutaka kujua anaendeleaje na maisha kila siku.
Hoyce Temu akimfariji mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi alipoitembelea familia hiyo mkoani Iringa. Ziara
hiyo nyumbani hapo ni kwa nia nzuri ya kutaka kujua jinsi
anavyokabiliana na changamoto za kila siku za maisha pamoja na watoto
wake wanne. Walizungumza mengi yakiwemo yale yanayomkwaza Bi. Itika Mwangosi na jitihada anazofanya ili kujikwamua.Aidha
Bi. Temu akiwa amewapakata watoto wa marehemu aliifariji familia hiyo
akiwataka kutokata tamaa na kuwa Mungu yupo na kwa kuwa watanzania ni
wamoja mambo yatakwenda sawa.
Hoyce Temu akiwapa kumbatio la upendo watoto wa marehemu Daudi Mwangosi.
Bi. Itika Mwangosi akionyesha uso wa matumaini baada ya kupewa maeneo ya faraja na Hoyce Temu. Amezungumza na watoto kuhusu kwenda shule na kutaka kujua wanasoma shule gani na iko umbali gani kutoka nyumbani. Pamoja
na mambo mengine Hoyce Temu kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania
amewasihi watanzania wenye moyo wa ukarimu kumsaidia Mjane huyo ambaye
hana ajira kwa hivyo ni vigumu kupata kipato cha kujitosheleza yeye na
wanawe kwa mahitaji muhimu ya kila siku.
Watoto wa Marehemu wakionyesha matumaini mapya baada ya kufarijiwa na Hoyce Temu.
Mtanzania
mwenye ufariji kwa familia hiyo anaweza kutuma kiasi chochote cha fedha
kwenye namba inayomilikiwa na mjane huyo Mama Itika Mwangosi kupitia
mtandao wa M-Pesa: 0767670739 ili msaada huo uwafikie walengwa.
Post a Comment