Hatimaye
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo
-Chadema Bw. Wilfred Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa
Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga
usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron
T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata
zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe,
Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe,
Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo.
Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa
matokeo usiku wa kuamkia leo saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba
ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Aron T. Kagurumjuli(Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini)
akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi
wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama
cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro
hicho baada ya kumwangusha mgombea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo
la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu.
Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Licha
ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa
zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika jumatatu
asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema
baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa Chadema
imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika
maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho
hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo
ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya
vijana hao ambao mpaka usiku walikuwa wamepandwa na jazba katika eneo
la ofisi za Halmashauri ya Bukoba. Vurugu zikiwemo kurushiana mawe
zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi
kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na
kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali
hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo
yakatangazwa.
Taarifa
zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili
ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa
Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu
kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa
kutosha.
Kura
zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni
805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na
asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura
25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Lwakatare wa Chadema amepata kura
28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi
wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri
Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Vingozi
wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna
Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika
Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei.
Bw.
Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa
Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri
ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA
Mwenyekiti
wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor
Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo
wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba
Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare
Wafuasi
wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za
Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa
wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo
mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa
ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia
chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.
Post a Comment