Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PICHA :RAIS MAGUFULI ALIVYOTUA ARUSHA JANA


RAIS John Magufuli ametoa mwito kwa Watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhirifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.

“Nataka niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa mafanikio,” alisema Dk Magufuli.

Alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha jana, alipotua kwa ziara ya kikazi ikiwa ni ya kwanza kwao tangu achaguliwe kushika wadhifa huo Novemba 5, mwaka jana.

Dk Magufuli aliwasili mkoani Arusha, ambako kesho atatunuku Kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani hapa.

Rais Magufuli aliwasili mjini Arusha akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es Salaam na kupokewa na mamia ya wananchi. 
Akiwa uwanjani hapo, Rais Magufuli aliwashukuru wananchi kwa mapokezi makubwa aliyoyapata na aliwaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi tu.

“Nawashukuru sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania kwa ujumla, ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake haitawabagua Watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa misingi ya vyama vyao na kanda zao. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro jana huku akiongozana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda tayari kwa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha itakayofanyika Januari 23 /2016. PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishiriki kupiga ngoma za utamaduni wakati alipowasili kwenye uwa nja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro jana
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi wakimpungia mikono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA mkoani Klimajaro.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top