Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

DKT KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA KIMATAIFA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA(OUT)


Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa jana Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa Shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.

“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt  Kikwete.

Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati  Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.

Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.

Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu 25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu chuo   kuanzishwa
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimpongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku Shahada  ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini  Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika  maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini  Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika  jana Jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Chuo Kikuu  Huria cha Tanzania  (OUT), Dk. Asha Rose Migiro akimhudhurisha Shahada ya Heshima ya Udaktari ya Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, katika mahafali ya 30 ya Chuo hicho, yaliyofanyika ana, Alhamisi, Januari 21, 2016, Kampasi  ya Kinondoni, Dar es Salaam. (Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog)
 Mkuu wa Chuo Kikuu  Huria cha Tanzania  (OUT), Dk. Asha Rose Migiro akimhudhurisha Shahada ya Heshima ya Udaktari  ya Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, katika mahafali ya 30 ya Chuo hicho, yaliyofanyika leo, Alhamisi, Januari 21, 2016, Kampasi  ya Kinondoni, Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo Kikuu  Huria cha Tanzania  (OUT), Dk. Asha Rose Migiro akimhudhurisha Shahada ya Heshima ya Udaktari  ya Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, katika mahafali ya 30 ya Chuo hicho, yaliyofanyika leo, Alhamisi, Januari 21, 2016, Kampasi  ya Kinondoni, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo Kikuu  Huria cha Tanzania  (OUT), Dk. Asha Rose Migiro akimpongeza baada ya kumhudhurisha Shahada ya heshima ya Udaktari ya Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, katika mahafali ya 30 ya Chuo hicho, yaliyofanyika leo, Alhamisi, Januari 21, 2016, Kampasi  ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Dk. Kikwete akishukuru
Dk. Kikwete akingoka baada ya kuhudhurishwa

 Dk. Kikwete akiwa na Rais wa Chuo Kikuu cha Choson cha Korea, Profesa  Such Chae Hong, ambaye naye pia alitunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari katika Mahahali hayo
 Dk. Kikwete na Profesa Such wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa Taifa  baada ya kutunukiwa Shahada zao za Udaktari. Kulia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro
 Dk. Kikwete na Profesa Such na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro
 Dk. Kikwete na Profesa Such wakiwa  Dk. Asha-Rose Migiro na viongozi wengie wa Chuo Kikuu Huria. Karibu na Dk. Migiro ni Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi
 Dk. Kikwete na Profesa Such wakiwa na Mama salma Kiwete na Dk. Asha-Rose Migiro na baadhi ya viongozi wa OUT
 Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Dk. Asha-Rose Migiro
 Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza mmoja wa wahitimu katika chuo hicho mwenye ulemavu wa miguu. 
 Dk. Jakaya Kikwete akimdodosa maswali, mtoto  Novatus Salala (11), ambaye alimuona akimpiga picha kwa simu wakati wa mahafali hayo. Kulia ni Mama Salma Kikwete 
 Dk. Jakaya Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu huria w zamani, Dk. John Malecela na Mkuu wa sasa wa Chuo hicho, Dk. Asha-Rose Migiri wakati akiondoka mwishoni mwa hafla hiyo.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top