Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MBWANA SAMATTA AZIDI KUNG'ARA ULAYA

Usiku wa April 20 2016 kocha wa KRC Genk Peter Maes kaendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuanza katika first eleven yake nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea klabu hiyo Mbwana Samatta, Maes amempa nafasi Samatta ya kuanza mchezo wa pili mfululizo.

Hii inatokana na jinsi Samatta anavyoonyesha kulizoea soka la Ulaya hivyo kuzidi kupewa muda zaidi wa kuwa Uwanjani.Kiwango cha Samatta pia kinachangia Kocha wake kumuamini kwani kila achezapo huonyesha uchu wa kufunga mabao na umakini uwanjani.

Licha ya kuwa KRC Genk walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Cristal Arena kukabiliana na vinara wa Ligi hiyo Club Brugge, Maes kamuamini Samatta na kumpa nafasi katika mchezo huo mgumu ulio malizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 4-2. Samatta amecheza kwa dakika 75 na dakika ya 76 alitoka akaingia Nikolaos Karelis.

 
sama 4
 Pichani ni kikosi kilichoanza katika mchezo huo

Samatta anakuwa amefikisha jumla ya mechi tatu alizoanza akiwa na KRC Genk katika mechi hizo amefunga mechi mbili goli moja moja katika kila mchezo, magoli ya KRC Genk ya leo yamefungwa na Onyinye Ndindi dakika ya 15, Alejandro Melero dakika ya 42, Thomas Buffel dakika ya 45 na Jeren Uronen dakika ya 73.
Screenshot_2016-04-21-01-14-18-1
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top