Na Dotto Mwaibale
Aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika jana jioni alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa lengo la kujua ni jinsi gani taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa moyo
waliolazwa katika Taasisi hiyo. pia
Mchezaji wa
zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye
pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwa katika Jengo
la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo jana. Kanu atakuwepo
nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni
na kijamii.
Akizungumza baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa
na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea
na kuahidi kubadilishana uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa
na wataalamu wa
tasisi hiyo.
“Tatizo la moyo ni kubwa sana kwa sasa na limekuwa likiongezeka kwa kasi
lakini cha kusikitisha ni kuwa sio kila mtu anaweza kumudu gharama za
matibabu yake. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali na wadau
wengine kuanzisha vituo maalumu kama hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.”
Alisema Kanu
Katika mazungumzo yake mchezaji huyo wa nyota wa zamani ambaye aliwahi
kuwika na vilabu kama vile vya Arsenal, Ajax na Inter Milan, amesema
kuwa pamoja na kuja kwa shughuli mbalimbali kama balozi wa kampuni ya
StarTimes lakini pia ana nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi
hiyo ya Moyo. Alielezea kuwa lengo ni kuwasaidia matibabu watoto wenye
matatizo ya Moyo ambao
wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.
“Nimefarijika sana kuona serikali ya watu wa Tanzania inachukua hatua
stahiki katika kuwasaidia wananchi wake. Pia ningependa kuchukua fursa
hii kuwataka watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima
afya zao mara kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata
matibabu na kupona.
Tumeona mifano michache ya wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika na
kwingineko duniani wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya mchezo
kutokana na kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha balozi
huyo wa StarTimes barani Afrika
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete, Dk. Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai
mwaka jana mpaka sasa tasisi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka
nje ya nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu mbali na kujizolea umaarufu na heshima kubwa katika medani
za soka barani Afrika na Ulaya yeye pia alifanyiwa upasuaji wa moyo
mwaka 1996 na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa
“The Kanu Heart Foundation.”
Taasisi yake hiyo iliyoko nchini Nigeria ambako ndiko alipozaliwa
aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya kusaidia wenye matatizo kama yake
na ameahidi taasisi hiyo kushirikiana na taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete katika masuala mbalimbali.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo
katika Taasisi hiyo, Dk Peter Kisenge (kushoto) akimkaribisha Nwankwo
Kanu Ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu
atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za
kampuni na kijamii.
Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akizungumza baada ya kufika Muhimbili.
Kanu (kulia), akizungumza na madaktari wa Taasisi hiyo.
Fatuma Shaban ambaye mtoto wake anatibiwa katika taasisi hiyo akipokea zawadi kutoka kwa mchezaji huyo.
Mgonjwa katika taasisi ya moyo ya
Jakaya Kikwete, Mariam Omary akifurahi baada ya kupata fursa ya
kutembelewa na kujuliwa hali na aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria,
Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani
Afrika.
Mmoja wa madaktari wa taasisi hiyo (kulia), akitoa maelezo mbele ya mchezaji huyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062
Post a Comment