Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU UJIO WA TB JOSHUA KUJA KUMUONA

Nashukuru kwa heshima aliyonipa mtumishi wa Mungu, T.B Joshua kwa kuja nyumbani kujadili mambo ya taifa, na baadaye kushiriki kwenye sala na ndugu na familia. Mungu atuongoze. Mungu ibariki Tanzania!"-Edward Ngoyai Lowassa
Maelezo kwa mujibu wa tovuti ya John Kitime (johnkitime.co.tz)Temitope Balogun Joshua (T.B. Joshua) alizaliwa tarehe 12 Juni 1963, katika kijiji kidogo cha Arigidi kilichoko Akoko, Jimbo la Ondo, Nigeria. Inasemekana mama yake alikaa na mimba kwa miezi 15, kabla Temitope hajazaliwa.

Katika kabila lake kulikuweko na hadithi ya zaidi ya miaka 100 ambayo ilitabiri kuwa kuna mtoto atazaliwa katika familia masikini, ambaye Mungu atamtumia sana, na wengi kule kwao huamini kuwa Temitope ndie aliyetajwa katika utabiri huo. Siku tatu baada ya kuzaliwa kwake, jiwe kubwa lilirushwa kutoka kwenye sehemu kulikokuwa kunapasuliwa mawe, jiwe hilo lilitoboa bati na kumkosa kosa Temitope kwa sentimita chache. Na ndipo mama yake alimpa jina la Temitope, likiwa na maana ‘Ulichonipa Mungu lazima kishukuriwe’.
Jina analojulikana sana sasa ni T. B. Joshua.

TB Joshua ni muhubiri mwanzilishi na kiongozi wa The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN), hii ni taasisi ya kidini inayoendesha Emmanuel TV, Tv ambayo huonekana kote duniani ikiwa inarushwa kutoka Lagos Nigeria. TB Joshua anasemeka ni moja ya watu 50 wenye ushawishi zaidi Afrika, anajulikana sana kwenye mitandao ya Facebook ambako anawafuasi zaidi ya milioni moja laki tano, na video zake nyingi zilizomo kwenye Youtube. Kwa mujibu wa Forbes, mwaka 2011 TB Joshua alikuwa mtu wa tatu kwa utajiri nchini Nigeria.

Wakati akiwa shule alijulikana kwa jina la Balogun Francis, alisoma shule ya St. Stephen’s Anglican Primary School ya Arigidi-Akoko, kati ya mwaka 1971 na 1977, lakini hakumaliza sekondari. Wakati yuko shule alijulikana kama “small pastor” kutokana na kupenda sana biblia, baada ya kuacha shule alifanya kazi mbalimbali ndogo ndogo, hatimae akaanzisha darasa la biblia kwa watoto, wakati huohuo akaanza kujiendeleza kwa masomo ya jioni. Hatimae akaamua kwenda kujiunga na jeshi la Nigeria, lakini kwa bahati mbaya akaachelewa treni kwenda kwenye usaili na hivyo ndoto hiyo ikaishia hapo.

Kwa maelezo yake mwenyewe anaeleza jinsi alivyokabithiwa upako wake, “ Nilikuwa katika hali ya kuzimia kwa siku tatu mfululizo, nikaona mkono ukielekeza Biblia kwenye moyo wangu, na Biblia ikaingia kwenye moyo wangu na moyo wangu wa zamani ukachanganyika na Biblia. Ufahamu uliponijia nikawaona Mitume na Manabii wa zamani wako na mtu ambaye sikuweza kuona kichwa chake kwa sababu alikuwa mrefu sana amefika mpaka mbinguni. Nikaamini kuwa alikuwa ndie Bwana wetu Yesu Kristo, nami nikajiona nimo katika hawa Manabii na Mitume wa zamani.
Nikauona mkono wa yule mtu mrefu sikuweza kuona uso wake maana ulikuwa na mwanga mkali sana sikuweza kabisa kuangalia uso wake. Lakini Mitume wengine niliweza kuwaona. Mitume Peter na Paul, Manabii Moses, Eliya na wengine, kwani majina yao yalikuwa yameandikwa kwa herufi kubwa vifuani mwao. Nikasikia sauti inasema, “Mimi ni Mungu wako, nakupa upako nenda kafanye kazi ya baba yako wa mbinguni.”
Wakati huohuo yule mtu mrefu akanipa Msalaba na Biblia iliyokuwa kubwa kuliko ile iliyoingia moyoni mwangu. Akaniahidi kuwa kila nitakapo tumia muda wake na jina lake nitapata Msalaba mkubwa zaidi, nikienda kinyume na mambo yatakuwa kinyume. Nikasikia sauti ya yule mtu mrefu ambaye sikuwa naweza kuona kichwa chake ikasema,’ Mimi ndie Bwana wako, niliyekuwa na ambaye ndie, mimi ni Yesu Kristo ninaetoa amri kwa mitume na manabii wote. Sauti ile ikasema tena ‘Nitakuonyesha mambo mazuri ya ajabu na nitajionyesha kupitia mafunzo, mahubiri, miujiza, ishara, kwa ajili ya kuokoa roho za watu. Kutoka wakati huo nimekuwa napata maono kila mwaka na Msalaba mkubwa zaidi ukiwa na maana majukumu makubwa zaidi”

SCOAN ina tawi moja tu nalo liko Ghana, kwa sasa kila Jumapili kuna ibada Nigeria ambayo huhudhuriwa na kiasi cha watu 15,000 kila Jumapili. Uponyaji ni kati ya mambo mengi yanayofanywa katika kanisa la TB Joshua watu wengi wamekuwa wakisema wamepona maradhi mbalimbali kutokana na kufika kanisani hapo na kwa kutumia maji, ‘annointed water’ ambayo hutolewa na TB Joshua.
Wakati wa tatizo la Ebola TB Joshua alisema maji hayo yanaweza kutibu ugonjwa huo na alituma chupa 4,000 za maji hayo zikiambatana na dola 50,000 kwenye serikali ya Sierra Leon. Hili lilikuja hasa baada ya maafisa afya wa Lagos walipomtembelea TB Joshua kumtaka asiwaruhusu wagonjwa Ebola kuja katika kanisa hilo kwa kuondoa uwezekanao wa kupata mlipuko wa ugonjwa huo katika jiji hilo. Wasanii wa Nollywood kama Jimmy Iyke na Camilla Mberekpe pia ni kati ya watu wengi waliowahi kupata huduma za kuondoa mapepo katika miili yao katika kanisa hilo.

Pia TB Joshua anasemekana ameweza kutabiri mambo mengi ikiwemo kifo cha Michael Jackson, milipuko ya Boston na hata matokeo ya mechi mbili za fainali za AFCON, ambapo moja mshindi alikuwa Zambia na nyingine Nigeria ilichukua ushindi. Amesha wahi kutabiri kuhusu kifo cha Rais mmoja wa Afrika na inasemekana Bingu Mutharika wa Malawi ndie aliyetabiriwa wakati huo. Pia anasemekana kutabiri kuhusu ndege ya Malaysian Airline iliyopotea baharini, miezi kadhaa kabla ya tukio hilo.

TB JOSHUA AZUA JAMBO BONGO .JE WAJUA NI NINI ?

TB Joshua Azua Jambo! Akanyaga Ardhi ya Tanzania Bila Viatu..Jambo lililoleta Maswali Mengi Sana Kwa Watanzania....Je Unajua Maana yake?

UJIO WA MCHUNGAJI TB JOSHUA WAZUA GUMZO MITANDAO YA KIJAMII BAADA YA KUTUA BONGO LIVE


Baada ya Ujio wa Mchungaji Maarufu Kutoka Nigeria TB Joshua Hapa Tanzania Siku ya Jana Kila mtu Anaongea yako kuhusu ugeni huo, Soma Hapa chini:


filbertmbwambo 
 Maswali magumu!
TB Joshua
1. Amekuja tz kushuudia kuapishwa kwa Magufu!?
2. Amekuja kuleta upatanisho!??
3. Amekuja kutoa maelekezo kuwa nani ni Rais halali??



mrekebishatabia
Ooh TB Joshua karibu tena na tena Tanzania...hata yeye pia hajakutana na EN Lowassa barabarani.
Tena bora amekuja maana nina list ndefu ya maombi maalumu. Huyu mtu nadhan si mchezo...si mnaona shati alilovaa?? Anafaa kabisa kutuombea watanzania hasa wenye mapepo ya Rangi mbali mbali.

udakutz_
TB Joshua baada ya kutua tu katika ardhi ya Tanzania alivua viatu na kanyaga ardhi ya bongo akiwa na soksi tu!! Hii ina maana gani?

linda_ukawa_supporter 
Naomba niwajuze kilichomleta TB Joshua kwa mujibu nilivyoelezwa na mtu wa karibu na Mbatia muda huu nikwamba kaja kunatafrija leo jioni na lengo lake kubwa ni kuwaeleza viongozi husika ukweli wa mambo kuwa mshindi wa urasis ni lowassa na km wanaweza wamuachie nchi maana kuna mapigo Mungu kamuonyesha kuwa watayapata kwa hiyo kaleta ujumbe wa Mungu ili kunawa mikono watakapo kaidi sauti ya Mungu.then km watakaidi pia wakimualika kwenye kumuapisha Magu atahudhuria km wageni wengine.maana yupo nchi kwa siku

mdaku_wa_town 
 IF THIS IS A STATE VISIT BASI LAZIMA SERIKALI ILIO IN POWER NDO IMPOKEE!. MIE SIMJUI HUYU JAMAA BUT NAISI NI MTU MWENYE POWER KWENYE AFRICAN SOCIETIES MIONGONI MWA VIONGOZI WA DINI. SO I GUES THATS WHY KAPATA MAPOKEZI YA KISERIKALI EVEN THOUGH KAJA KUTOA MESSAGE YAKE......PLUS HE WAS MORE COMFORTABLE KWA LOWASA KULIKO IKULU. CCM NI KUJISHAUWA TU WAMEMPOKEA BUT HAKUJA KI CCM. NI MAMBO YA PROTOCOL
Read more at http://websta.me/n/mdaku_wa_town#qRZiIzo8l0ig9zmj.99

TB JOSHUA KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS DR MAGUFULI

Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa
 ( Picha na Ikulu)

Na Mwandishi WETU Dar 
Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria, ametua Jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuja kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli.

Mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, TB Joshua alikwenda moja kwa moja Ikulu, kumsalimia Rais Jakaya Kikwete.

Katika mazungumzo yao, TB Joshua alimpongeza Rais Kikwete kwa kufanikisha uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, ambao alisema ulifanyika kwa uhuru na amani.
Alimweleza Rais Kikwete kuwa, kutokana na kufanikisha uchaguzi huo, anaondoka madarakani kwa furaha na amani.
Aidha, alimpongeza Rais Kikwete kwa kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumpata Dk. Magufuli kuwa raia wa awamu ya tano.
Alimwelezea Dk. Magufuli kuwa ni Rais wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top