Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MKUU WA WILAYA AMZUIA WAZIRI KWENDA KIJIJINI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, juzi alimzuia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba kwenda kijiji cha Mikomario wilayani Bunda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji kwa madai ya wasiwasi wa usalama kuwa mdogo.

Baada ya jitihada zake za kumzuia kugonga mwamba, Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda aliamua kujitenga na ziara hiyo kwani licha ya kufika eneo la mkutano, hakujihusisha na lolote kwa kuamua kukaa pembeni.

“Mheshimiwa waziri nakushauri usiende Kijiji cha Mikomario kwa muda huu ambao unakaribia usiku kwa sababu usalama utakuwa ni mdogo kutokana na ukorofi wa wananchi wa eneo lile,” alishauri Nyamubi wakati akizungumza na Nchemba ofisini kwake.

Hata hivyo, waziri Nchemba alisisitiza kuwa lazima aende kuzungumza na wananchi hata kama atalazimika kuhutubia kwa kutumia taa za gari kwa sababu aliwaahidi kuwa angefika na kuzungumza nao na walikuwa wakimsubiri tangu mchana.

 “Mheshimiwa kaimu mkuu wa mkoa, bado sijashawishika kutotimiza ahadi ya kwenda kuzungumza na wananchi wale, wamenisubiri tangu asubuhi na nimepata taarifa wako uwanjani hadi jioni hii wakinusubiri. Kutokwenda ni kutowatendea haki,” alisisitiza Nchemba.

Baada ya msimamo huo, ndipo Nyamubi alipotangaza kujitoa kwa lolote ambalo lingetokea, licha ya kuwamo kwenye msafara wa viongozi uliofika kijijini hapo saa 12.40 jioni, hakukaa meza kuu wala kujishughulisha na lolote hadi mkutano ulipomalizika kwa amani saa 1.10 usiku.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ambacho kimekuwa na mgogoro wa ardhi kwa miaka 30 sasa bila ufumbuzi, Waziri Nchemba aliahidi kuutafutia ufumbuzi, lakini akawasihi kuwa na subira kwa sababu lazima awasiliane na wizara nyingine zinazoguswa nao.

“Suala hili ni la kisheria, hivyo linatakiwa kutatuliwa kisheria badala ya mapigano, nipeni fursa ili wizara yangu iwasiliane na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Tamisemi ili kwa pamoja tuutafutia ufumbuzi.

“Wenye mamlaka ya kupanga na hata kubadili matumizi ya ardhi ya kijiji ni ninyi wananchi kupitia mikutano na Serikali yenu ya kijiji, viongozi na wataalamu kazi yetu ni kutoa ushauri kuhakikisha uamuzi wenu unakuwa halali,” alisema.

Wakiwa na mabango yenye ujumbe, wakazi hao walimpongeza waziri kwa kutimiza ahadi ya kuzungumza nao ili kutafutia ufumbuzi mgogoro huo unaohusu hekta 2, 500 zinazodaiwa kutolewa kwa mwekezaji bila ridhaa ya Serikali ya Kijiji.

FIELD MARSHALL MWIGULU NCHEMBA ATUA KIJESHI MVOMERO KUTAFUTA SULUHU YA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

 

Mh:Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.

 


Mh;Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.

Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.

 

Mh:Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero. 

Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga. 

Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa. 

Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga  na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda. 

Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero. 

Mwigulu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.

 


Waziri wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.
Picha na Sanga Festo Jr.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top