Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI MWIGULU:TUNASONGA MBELE




Tunasonga mbele,Asante Mh. Rais J.P.Magufuli kwa hatua kubwa hii ya kuzindua hati ya kusafiri ya kielektroniki.Mkataba wetu na watanzania ni kuwaletea maendeleo chanya kadri Mungu atakavyotujalia.

WAZIRI KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI, AWATAKA WAPANGE MIKAKATI MIPYA YA KUPAMBANA NA WAHALIFU NCHINI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Jeshi hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao kutoka mikoa yote nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
 Sehemu ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam kabla ya waziri huyo kuufungua Mkutano huo wa Mwaka wao wa Mwaka kwa ajili ya kufanya tathimini ya utendaji wao pamoja na kuliboresha zaidi Jeshi hilo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiyajibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari ambao walitaka kupata ufafanuzi zaidi kutokana na hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. 

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA VITUO VYA UHAMIAJI VYA MIPAKANI MKOA WA KILIMANJARO

Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.
Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden Mwakalobo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAANZA KAZI RASMI - YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akijitambulisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya Wizara hiyo katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo baada ya kuundwa na Bunge hivi karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali Masoud Khamis. Kulia kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao chao kwanza tangu Kamati hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kanali Masoud Khamis. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akitoa taarifa ya Wizara katika kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa Wizara, kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (hayupo pichani) alipokuwa anawasilisha taarifa ya Wizara kwa Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira wakiiweka sawa taarifa ya wizara yao kabla ya kuiwasilisha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Watendaji wa Wizara walikutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WINGU ZITO MABILIONI NIDA



Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam 
*Matumizi ya bilioni 179.6/- hadharani.

*Kila kitambulisho chatafuna Sh 89,800

Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam


WINGU zito limetanda ndani ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu matumizi ya  Sh bilioni 179.6 ambako kila kitambulisho  cha taifa kimegharimu Sh 89,800 zikiwamo gharama za utawala, MTANZANIA limebaini.


Hayo yamebainika  siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kushangazwa na watendaji wa mamlaka hiyo ikizingatiwa vitambulisho vilivyokwisha kutengenezwa hadi sasa havifiki   milioni mbili na havina saini.


“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina.  Wapo watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana  wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.


“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara wa Sh milioni 35 kwa mwezi…naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.


Rais Dk. Magufuli, licha ya kushangazwa na hali hiyo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipewa Sh bilioni 70 lakini iliweza kutengeneza vitambulisho   23,253,982 ambavyo vilikuwa na saini ya kila mpiga kura na kila kimoja kimegharimu Sh 3,010.


Kutokana na hali hiyo, tofauti ya gharama kati ya kitambulisho kimoja cha NIDA na cha NEC ni Sh 86,790.


Pamoja na hayo, hivi sasa Watanzania wanasuburi   ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, kuhusu  matumizi ya fedha hizo za NIDA.


Januari 26 mwaka huu, Rais Magufuli alitangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi yake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu.


Maimu alisimamishwa kazi pamoja na maofisa wengine wanne, kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali.


Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.


Akitangaza uamuzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alisema taarifa zilizomfikia Rais zinaonyesha kuwa NIDA hadi wakati huo ilikuwa imetumia Sh bilioni 179.6, kiasi ambacho ni kikubwa.


Alisema Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi kujua jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.


Licha ya kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, afanye ukaguzi maalumu wa hesabu za NIDA  ukiwamo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa, pia aliitaka Takukuru ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

Historia ya NIDA
Mradi wa Vitambulisho vya Taifa umekuwa na historia ndefu. Ulibuniwa mwaka 1972 ikiwa ni  zaidi ya miaka 38 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya mwaka 1972.


Tangu wakati huo, mawaziri   waliopita Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali  ikiwamo mgongano wa masilahi ya umma na ya binafsi.


Oktoba 1999 mradi huo ulitangazwa na kampuni 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za ufisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.


Serikali iliipa kazi hiyo kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na Ofisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia ‘mchanganuo’ wa mradi huo.


Mabilioni yanavyopotea
Ripoti mbalimbali zinaonyesha  Serikali imepoteza karibu  Sh bilioni 500 kwa   miaka tisa  kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma  ikiwamo rushwa na ubadhirifu wa mali mbalimbali.


Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia  katika moja ya ripoti zake alizowahi kuzitoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba.


“Katika kipindi kisichozidi miaka tisa kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake zimelisababishia Taifa hasara ya karibu Sh bilioni 500 ambako kwa wastani inapoteza takriban asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka,” alisema Sungusia.


Alizitaja kashfa hizo kuwa ni   mabilioni ya shilingi kupitia ununuzi wa rada iliyotumika kutoka Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza, wizi wa mabilioni katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) na kashfa ya mabilioni ya fedha walizogawiwa baadhi ya viongozi wa uuma, kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA KUWATAKA KUBUNI MIRADI MBALIMBALI YA KUONGEZA MAPATO NDANI YA JESHI HILO



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo (Kushoto), akisalimiana na Maofisa  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Braiton Manyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, taarifa ya ujenzi la Jengo laa  linalotarajiwa kuwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizoko TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza  na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizopo TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wa tatu kutoka kulia waliokaa),akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea makao Makuu ya Jeshi hilo na Ofisi zilizopo Tazara,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).


Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya  Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA IDARA YA UHAMIAJI KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM – AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI MPYA

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa  ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
 Afisa Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi  taarifa za muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa hati za  kusafiria,  Amir Hassan (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),moja ya pasi iliyokua imeshachapwa tayari kwa matumizi ya kusafiria, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Uhamiaji (Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi), Victoria Lembeli (katikati), akimuonesha  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, moja ya karatasi iliyokataliwa na mfumo wa komputa baada ya kubainika kwa taarifa za uongo za muombaji wa Hati ya Ukaazi, wakati Naibu Katibu Mkuu  huyo alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini,jijini Dar es Salaam.
 Maafisa wa Idara ya Uhamiaji, wakimsikiliza  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani), alipofanya mkutano nao wakati wa ziara aliyofanya  Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Silvester Ambokile akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya machapisho ya Idara ya Uhamiaji, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai) katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wapili kushoto mstari wa mbele, ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top