Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Daladala Time:Kama Kawaida dereva wanavyowazuga askari barabarani ila Bonge huyu kazidi hata shati lake mwenyewe Tatizo

Akiwa katulia hana papara bila ya sare ya kazi hapo ni mpaka amuone askari wa usalama barabarani ndio unachukua sare yake hapo mbele ya dashibodi kama uionavyo hapo rangi ya blue huku hata shati lake likiwa ni shida kufunga vifungo kama inavyoonyesha dereva wetu hapo.



Sare kaziweka kwenye dashibodi ya gari mbele hapo kama taswira inavyoonyesha sare hizo zikiwa zimewekwa hapo huku zikiwa hazijulikani zilipata sabuni lini zikiwa na hali ya uvundo.
Ni Maarufu kwa jina la utani Bonge kama tulivyosikia wakiitana yeye na kondakta wake ni Leo asubuhi daladala ifanyayo safari yake kati TABATA SEGEREA-UBUNGO akiwa makini kwenye usukani wake huku akiwa kavaa kofia yake kichwani na shati la drafti ambalo sio sare wanayotakiwa kuvaa wawapo kazini.Sare kaziweka kwenye dashibodi ya gari mbele hapo kama taswira nyingine zinavyoonyesha.
Bonge nini tenaa hapo !! Hapo keshaona dalili za askari barabarani mbele hivyo akachukua sare yake na kuvaa mkono mmoja ili kuzuga kama wasemavyo vijana wa mjini ili aonekane kavaa sare kumbe ndivyo sivyo.Lakini kama uonavyo ''Bonge'' akiwa hata shati lake mwenyewe likiwa ni shida kulifunga vifungo na vikiwa vimepishana vilivyofungwa..Daladala Time hapa hapa Rundugai Blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top