Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Daladala Time:dereva aianza siku kwa ''kuvurugwa'' .

Kama ilivyo ada kwa madereva wa daladala kutovaa sare yao wawapo kazin,dereva huyu afanyae safari kati ya Tabata Segerea-Kariakoo/Mnazi Mmoja alionja shubiri pale alipojikuta uso kwa uso na Askari wa Usalama Barabarani.Hapo anaonekana hajavaa sare yake huku akipiga mzigo kama kawa ni asubuhi na mapema kila mmoja akijaribu kuwahi eneo lake la kazi lakini kabla hajaanza kulitafuta shati liko wapi dereva huyo akajikuta akiangukia mikononi mwa askari.
Akiwa hoi bin taabani kwa makosa aliyoandikiwa na askari huyo wa Usalama barabarani ni dhahiri kesha choka kwa makosa yaliyopatikana kwa yeye kutovaa sare pamoja na gari analoendesha kutokidhi viwango.Akaamua kulitupia tu shati hata kulivaa vizuri akaona shida maana siku itaisha kutafuta fedha ya kulipia faini.Je fedha ya tajiri pamoja na posho yao ya siku wataipateje ?

Aliongea neno moja ''Tushavurugwa''
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top