Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Daladala Time:Swaggazz za Kondakta

Shati likiwa limekunjwa kola hapo uvaaji ni ilimradi anaonwa ana sare ya kazi

Kofia kubwa kichwani ikiwa imeegeshewa na ''mjanja'' huyu mwingi wa maneno alikuwa haiishi ongea na abiria wake.


Mkononi sasa ni mwendo wa kutii kiu yako hapo anapata ''fanda'' taratiibuu
Shughuli ikaanzia hapa alipotoa fedha mfukoni na kuanza kuzihesabia maana mida imeyoyoma sasa tajiri lazima chake salio apewe,sarawili nayo hiyooo..!!!
Haikubali kukaa mahala pake maana toka mwanzo ilionekana imeegeshewa tu ili wale maafisa wa usalama barabarani wakimuona wanajua ''Bingwa'' kavaa sare hana neno,kumbe ! Geresha tu.
Soda nayo kumbe kabebeshwa abiria ,Dada na gauni la kitenge soda mkononi kwenye daladala . kazi ya konda hiyo.
Hapoo sasa sarawili inakataa kazi hapo inalazimishwa tu na miguu lakini kiuhalisia yenyewe ilitaka kushuka kabisa imuache konda na hiyo draftii yake !!
Hapo akaona isiwe shida akaifuata ilikokimbilia na kuipandisha ili iweze msitiri japo kwa muda.
Hizo ni taswira za kondakta afanyae kazi zake njia ya Bugurui-Posta ambae uvaaji wake wa Sare ulikuwa bora liende tu kama ilivyo kwa baadhi ya makondakta ambao wengi hawapendi kuvaa vizuri sare zao za wawapo kazini.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top