Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012:VIGOGO WATEMA CHECHE

 Mhe.Edward Lowassa(Mbunge wa Monduli)
 
WAKATI Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiinyooshea kidole Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za kata, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema hatajiuzulu ng’o kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.

Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), nalo limetishia kuitisha maandamano ya nchi nzima kwa kushirikisha wanafunzi wote waliopata sifuri ikiwa waziri huyo hatajiuzulu.

Taifa limeshikwa na mshtuko kutokana na matokeo hayo ambayo yanaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo mwaka jana, walipata sifuri.

Dk Kawambwa
Akizungumza jana katika uzinduzi wa Mpango Maalumu wa Mafunzo ya Kompyuta katika Shule ya Msingi ya Majengo wilayani Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema hawezi kuachia ngazi kwa shinikizo la wanasiasa.

Alisema yeye si wa kulaumiwa kutokana na wanafunzi hao kufanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha nne na kwamba wanaosema waziri anapaswa kujiuzulu hawana hoja za msingi zaidi ya kutaka kujipatia umaarufu kwa kudandia hoja zinazokuwapo kwa wakati husika.
“Unajua katika mfumo wa vyama vingi, kila linapotokea jambo baya basi wanaona dawa ni kiongozi mhusika kung’oka. Unapozungumza waziri kujiuzulu hiyo ni lugha ya kisiasa lakini hata akijiuzulu inakuwa bado tatizo halijaweza kupatiwa ufumbuzi,” alisema.

Dk Kawambwa alisema hata Serikali haijafurahishwa na matokeo hayo mabaya na kushauri njia nzuri ni kutafuta dawa ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kufeli huku akiahidi kuwa wizara yake inaangalia tatizo hilo kwa karibu zaidi ili kujua chanzo chake.

Alisema amesikitika kuona hata shule ambazo zilikuwa zinategemewa kufanya vizuri zikiwamo za seminari, watu binafsi na kongwe za Serikali, nazo zimefanya vibaya.
Aliunga mkono maoni ya kutaka mfumo mzima wa elimu nchini uangaliwe upya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa elimu.


Lowassa
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lowassa alisema matokeo hayo ni aibu kwa taifa na kuilaumu Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za kata.
Alisema taifa kwa sasa linazalisha wabeba kuni na maji na siyo wasomi ambao wanaweza kushindana kwenye soko la ajira.

Alisema sekondari za kata ambazo zilianzishwa chini ya usimamizi wake akiwa Waziri Mkuu, zilikuwa ukombozi kwa Watanzania wengi wa kipato cha kawaida na ndiyo sababu waliitikia wito kwa kuchangia ujenzi, hatua ambayo alisema ilimpa faraja kubwa.

“Serikali tuliahidi kuzikamilisha shule hizo kwa kuzijengea maabara na kuhakikisha zina walimu. Ni wajibu wake kutimiza. Mimi ndiyo maana hata kwenye Katiba Mpya nilipendekeza uwezekano wa elimu ya sekondari kuwa bure, elimu ni kama mapigo ya moyo ya taifa ukiona hayaendi vyema lazima ujiulize,” alisema.

Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, alisema tangu aondoke madarakani, shule hizo nazo zimetelekezwa.

Alimwomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua za makusudi, ikiwa ni pamoja na kuunda tume ili ichunguze kwa makini kiini cha matokeo hayo mabaya.

“Matokeo hayo ni aibu kwa taifa, walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe. Namwomba kwa dhati Rais afanye kitu cha ziada, natambua mchango wa juhudi zake katika sekta nyingine ikiwamo ujenzi wa barabara nchini lakini elimu ndiyo iwe ya kwanza,” alisema.

Alitaka ufike wakati nchi iamue kuwekeza katika elimu tofauti na ilivyo sasa kwa Tanzania kuwa nchi inayotenga fedha kidogo zaidi katika sekta hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


 Alisema Tanzania inatumia asilimia 1.4 ya bajeti yake, Kenya asilimia saba, Rwanda 5.8%, Uganda 4.8% na Burundi ni 3.2%.

Bavicha na maandamano
Bavicha imetishia kuitisha maandamano hayo yatakayowahusisha wanafunzi wote waliofeli ikiwa Waziri Kawambwa hatajiuzulu ndani ya siku 14 kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alivyomtaka Jumanne wiki hii.


Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bavicha, Deogratius Munishi alisema wameshaanza kuwajulisha viongozi wa mikoa na wilaya kuhusu taratibu zote za kuandaa maandamano hayo.

Alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kutaka kushinikiza pia Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule za Sekondari wa Wizara ya Elimu kujiuzulu ili kupisha wengine watakaosimamia kikamilifu mabadiliko ya mfumo wa elimu nchini.

“Tunaitaka pia Serikali ya CCM ieleze hatima ya maisha ya vijana waliofelishwa na mfumo mbovu wa elimu,” alisema na kuongeza kuwa kuna wanafunzi 800,000 waliofeli ambao wako mitaani tangu tatizo la matokeo ya kidato cha nne lilipoanza mwaka 2009.
Alisema Serikali ya CCM ilikuwa na lengo la ufaulu wa asilimia 70 kwa kidato cha nne tangu mwaka 2009 lakini imekuwa kinyume chake.

“Ukweli usiofichika ni kuwa Serikali ya CCM haiwezi kufikia lengo la kuwa na taifa lililoelimika ifikapo 2025 kama ilivyobainisha kwenye dira yake ‘Vision 2025’ na badala yake itajenga taifa la watu mbumbumbu kwa wakati huo,” alisema.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

3 comments

Kama ningekuwa mtu mwenye maamuzi ningefanya mambo haya:
1. Mtihani urudiwe au usahihishwe upya
3. Ningefumua wizara na kuunda tume kuandaa mitaala mipya

Reply

ilivyokuwa zanzibar wanafuata mtaala wao hadi form 3 ,zanzibar itunge mitihani yake

Reply

ELIMU ZANZIBAR

Assalam Aleykum!

Nina wingi Heshima kuleta Barua hii kwko ili izingatiwe kwa Manufaa ya Nchi yetu. Hivi Karibuni tumepata kusikia majibu ya Wanafunzi wetu waliofanya Mtihani wa O level.Kwa kiasi kikubwa tumepiga hatua khasa kwa School ya Lumumba kwa kuwa ni mojawapo ya School iliofanya uzuri Tanzania. Pia Wanafunzi wengi wameweza kufukia khatua hii ukilinganisha na siku za Nyuma. Mashallah , tumepiga khatuwa!

Ninashukuru wale wote waliofanya jitihada hii kwa mafanikio hayo.Mwenye Enzi Mungu atawajaalia Malipo mema duniani na kesho mbele ya Haki! Ameen!

Kuna baadhi hawakufanya uzuri na kuna baadhi mitihani imefutwa kutokana na sababu mbali mbali. Naomba kuchukuwa Fursa hii kukuomba ufanye JITIHADA wasamehewe na wapewe fursa ya Kurudia Mtihani kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu ili wwawahi kuingia Form V . Hii pia ingewezekana Wizara yako ikawadhamini kwa kutunga Mtihani mbadala kwa Zanzibar ili hili lifnikiwe.

Tukumbuke kuwa ELIMU ni Ufunguwo wa Maisha .Ni wajibu wetu kushirikiana na wadau husika wa Elimu tuufanye ili tutoe quality Education hapa Zanzibar. Ninatumai Ofisi yako inafanya kila Jitihada kumaliza matatizo ikiwemo mitaala , walimu ,vifaa na mazingira ya School zetu.

Haya yote yanawezekana kutatuliwa khatua kwa khatuwa.

Nafikiri ilivzokuwa sasa tunazo University ya kutosha ,tuanze kutowa Mitahani yetu wenyew hatimae tuwe Wadau kwenye Mitihani ya Afrika Mashariki siku zijazo au Taasisi za Elimu za Kimataifa . Hili linaweza kufanyika sambamba na Mfuomo wa Mitihani ya Taifa kama baadhi ya Shule zinavyoendesha Mitihani ya Taifa na ya Cambridge pia.

Nakumbuka 1970 , Zanzibar ilitowa Mtihani wake wa Zanzibar Certificate ya O level na ya A Level . Wakati huo tulikuwa hatuna University Zanzibar lakini hili liliwezekana.Turekebishe matatizo kwenye Walimu wenyewe na mfumo wa Elimu yaani Mtaala.

Hili la Mtaala huenda likachkukuwa muda lakini ili la walimu ni process ndogo tu ambayo sio ya kuongeza FEDHA bali
kuleta Education Inspection na Performance Indicators kwa Walimu,Wanafunzi na Maafisa wa Wizara husika.

Ni wajibu wetu pia kuhakikisha kuwa Syllabus
imesomeshwa na kuwapa wanafunzi matayarisho ya Mitihani mpaka tutakopweza kuwa Mitaala muwafaqa. Sasa hivi Kriteria ni kupasi form IV au Form VI .n.k ikiwa mwanafunzi amejifunza kupasi au amejifunza
elimu bila kujali ameinywa masuali au la. Khatua ya pili kuwa na Mtaala ambao utategemea UWEZO wa kujifunza badala ya uwezo wa kukariri.

Sasa tuanze dual approach yaani mwanafunzi awe anaweza
kufanya Zanzibar Exam national ya Tanzania kama school zengine zinavyofanya London GCE na National ya Tanzania.
Walimu wote wapewe mafunzo ya quality education na promotions zao zitegemee utendaji wa wanafunzi badala ya miaka kazini .

Wakati pia umefika Zanzibar kuleta Appraisal Oriented Incentives yaani Motisha kwa mujibu wa mafanikio kwa Walimu.

Nakutakia Afya Njema, Umri Mrefu na Kheri katika Ujenzi Wa Taifa.

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top