Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TATHMINI:LOWASSA AMEMFUNIKA DR.SLAA



UCHAGUZI Mkuu wa Tanzania umeisha kwa  Dr.John Pombe Magufuli kutangazwa mshindi.Lakini Pamoja na kutoshinda kwa Ndugu Edward Ngoyai Lowassa, bado kuna haja ya kufahamu kuwa Lowassa amemzidi na kumfunika Dr. Slaa aliyegombea mwaka 2010 kupitia CHADEMA.


Mwaka 2010, kura zilizopigwa zilikuwa 8,398,394 na Dr. Slaa alipata kura milioni 2.2 ambazo ni sawa na asilimia 26.34 ya kura zote.Na uchaguzi haukuwa na msisimko mkali kama huu wa Mwaka huu,ambapo zilipigwa kura 15,193,863 na Lowassa kupata kura milioni 6 na ushee sawa na asilimia 39.97.


Mshindi wa mwaka 2010,Rais Kikwete alipata asilimia 61 na wa mwaka huu amepata asilimia 58.46. Ukitazama kwa jicho kali, utaona na kujua kuwa Lowassa amemzidi kwa mbali sana Dr. Slaa. Pia, CCM imeendelea kupungua kwa asilimia za kura zake. Ni wazi sasa kuwa, Lowassa ameongeza hata majimbo ya uchaguzi kwa CHADEMA na CUF pamoja na vyama hivyo kupoteza baadhi ya majimbo yao.

Lowassa amesaidia kupoka ngome mbalimbali za CCM na kuzikabidhi CHADEMA na CUF. Mwaka huu, kwa uwiano wa kura za wagombea wa Urais wa Tanzania, CHADEMA itapata nafasi za viti maalum kwa wingi zaidi na kutoachwa mbali na CCM kama ilivyokuwa mwaka 2010. Haya pia ni mafanikio yaliyoletwa na Lowassa huko CHADEMA na kumzidi kwa mbali Dr. Slaa wa mwaka 2010. CHADEMA ilicheza karata zake vyema.

Tupia maoni yako kuelezea tathmini yako kutokana na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu 2015.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

2 comments

kama tutachagua 2020 hawana chao

Reply

kama tutachagua 2020 hawana chao

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top