Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mikwaju ya Penati yaiondoa Ureno






Ni Mabingwa watetezi Uhispania ambao wameingia fainali ya EURO 2012,hiyo ni baada ya kumalizika kwa dakika 90 na zile za ziada dakika 30.Hivyo mchezo kumalizwa ubishi kwa changamoto ya mikwaju ya penati ambapo waliishinda Ureno magoli 4-2.

Alikuwa Cesc Fabregas alietumbukiza kwenye kamba mkwaju wa mwisho hivyo kuwapa matumaini ya kuweza kutetea Ubingwa wao vizuri watakapo kutana na Ujerumani au Italia katika Fainali itakayochezwa Jumapili.

Fabregas kiungo mahiri wa timu ya Barcelona ndie alipiga penati ambayo baada ya kugonga mwamba kushoto ilitambaa na mtambaa wa panya kama unavyojulikana na kujaa kwenye kamba hivyo kuwapa tiketi ya Fainali hapo katika mji wa Kiev nchini Ukraine kwa ajili ya mpambano wa Fainali inayotazamiwa kuwa ya kukata na shoka.


Kwa upande wa Ureno alikuwa Mchezaji Bruno Alves alieonekana kuwa na mchecheto toka anaenda kupiga mkwaju wa penati na kushindwa kufunga kwa mpira kugonga mwamba hivyo kumfanya hata mchezaji mashuhuri Ronaldo ambae alitakiwa kuwa wa mwisho kupiga penati kushindwa kupiga penati hiyo kwani isingeweza kuleta mabadiliko yeyote.

Joao Moutinho mkwaju wake nao uliokolewa na golikipa mahiri wa Uhispania Casillas ambae aliruka upande wa kulia na kufanikiwa kuokoa penati hiyo ya Mreno huyo.

Kwa Upande wa Uhispania Xabi Alonso alikosa baada ya kipa wa Ureno Rui Patricio kuzuia shuti kali la Mhispania huyo.

Portugal: Rui Patricio; Joao Pereira, Pepe, Bruno Alves, Fabio Coentrao; Meireles (Varela 113), Veloso (Custodio 106), Joao Moutinho; Nani, Almeida (Nelson Oliveira 81), Ronaldo.

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Eduardo, Quaresma, Ricardo Costa, Rolando, Ruben Micael, Miguel Lopes, Hugo Viana, Postiga, Beto.

Waliopewa Kadi: Fabio Coentrao, Pepe, Joao Pereira, Bruno Alves, Veloso.

Uhispania: Casillas; Arbeloa, Pique, Sergio Ramos, Jordi Alba; Busquets, Alonso; Silva (Jesus Navas 60), Xavi (Pedro 87), Iniesta; Negredo (Fabregas 54).

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Valdes, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Torres, Mata, Llorente, Santi Cazorla, Reina.

Waliopewa kadi: Sergio Ramos, Busquets, Arbeloa, Alonso.

Refa wa mechi: Cuneyt Cakir (Turkey)

Walioingia Uwanjani: 51,500.




author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top