Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Wananchi CUF akerwa na kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa


KAULI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUWA ATAVIFUTA BAADHI YA VYAMA VYA MIFUKONI "POCKET PARTIES" NI YA KINAFIKI KWELIKWELI, NI KAULI INAYOUDHI NA KUSIKITISHA.

CHANZO CHA KUWEPO VYAMA VYA SIASA VYA MIFUKONI NI YEYE MWENYEWE MSAJILI, KAULI YAKE YA KUTAKA KUVIFUTA VYAMA HIVYO INAMSUTA,HAITEKELEZEKI NA INAMTIA AIBU.

TAIFA LETU LIMEFIKA MAHALI AMBAKO WAZEE AMBAO TUMEWAKABIDHI OFISI ZA UMMA WANAONGEA UONGO HADHARANI.

KUNA MAKUSUDI YA WAZI YANAYOAMBATANA NA UJANJA NA HADAA KUBWA ZINAZOFANYWA NA OFISI YA TENDWA HUKU YEYE MWENYEWE AKIHUSIKA KWA ASILIMIA MIA MOJA KATIKA KUHAKIKISHA VYAMA DHAIFU VISIVYO NA VIGEZO VINASAJILIWA.

MKAKATI HUU UNAFANYWA KWA LENGO LA KUWEKA UTITIRI WA VYAMA AMBAO HUGEUKA KUWA MAWAKALA WA KUISAIDIA CCM KATIKA CHAGUZI.

NDIYO MAANA HATA KWENYE UCHAGUZI WA MWAKA 2010 KUNA VYAMA KADHAA VILITANGAZA WAZIWAZI KUMUUNGA MKONO RAIS KIKWETE NA VIKAZUNGUKA NCHI KUMPIGIA KAMPENI.

LEO "MSAJILI WA VYAMA" ANAZUNGUKA KUWAHADAA WATANZANIA KUWA ATAVIFUTA VYAMA HIVYO, HUU NI UZUSHI NA UONGO MKUBWA. TENDWA HAWEZI KUVIFUTA VYAMA DHAIFU ALIVYOVISAJILI YEYE MWENYEWE ILI KUTEKELEZA MKAKATI WA KUISAIDIA CCM.

TUMECHOKA KUWA NA UONGOZI WA KINAFIKI NA UNAOTUMIA OFISI ZA UMMA KWA AJILI YA MATUMBO YAO HUKU WATANZANIA WAKITESEKA KWA UMASIKINI WA KUTISHA.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA ICHUNGUZWE, KUNA MASHAKA MAKUBWA NA HATA VIASHIRIA VYA UFISADI KATIKA USAJILI WA BAADHI YA VYAMA VYA MIFUKONI, TAKUKURU WAINGIE KAZINI, TENDWA NA OFISI YAKE WACHUNGUZWE, BINGE LIFUATILIE SUALA HILI PIA.

JULIUS MTATIRO,
NAIBU KATIBU MKUU,
CHAMA CHA WANANCHI CUF - TZ BARA,
24.06.2012.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top