Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Ujerumani yaiduwaza Ugiriki yatangulia Nusu Fainali





Ilikuwa usiku wa Jana katika uwanja wa PGE Arena, Gdansk, nchini Poland,Pale Ujerumani ilipoiduwaza Ugiriki kwa kuichapa magoli 4-1 la Ugiriki na kutangulia Nusu Fainali katika Mashindano yanayoendelea ya EURO 2012 katika mchezo huo wa Robo Fainali ya Kuvutia.

Baada ya kosakosa za hapa na pale katika dakika za Mwanzo alikuwa ni Kapteini Philipp Lahm beki mahiri aliepanda mbele na kupiga Mkwaju toka yadi 20 na kuipatia bao safi timu yake hiyo katika dakika ya 39 bao hilo lilimsimamisha toka kwenye kiti Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na kushangilia bao hilo.

Bao hilo la Kapteini wa Ujeruma Lahm lilidumu hadi kipindi cha pili ambapo mnao dakika 55 Ugiriki ilizinduka na kupata bao safi toka kwa mchezaji Georgios Samaras hivyo ngoma kuwa mbichi kabisa.

Lakini bao hilo lilikuwa kama la kuwazindua Ujerumani ambao kunako kupitia Mchzaji wao Khedira dakika ya 61 aliipatia Ujerumani bao la pili Kabla ya Mchezaji anaetisha kwenye timu hiyo Klose kuipatia Ujerumani bao la tatu dakika ya 68.

Mabao hayo yote yalikuwa yakipokelea kwa furaha kubwa na Kiongozi wa Ujerumani ambae alikuwa na wakati mwema dakika zote za mchezo kutokana na kandanda lililokuwa likionyeshwa na vijana wake.

Huku Ugiriki wakionekana kabisa kupoteana uwanjani walipigwa bao la nne na mchezaji Reus katika dakika ya 74 ya mchezo.

Mchezaji wa Ugiriki Dimitris Salpingidis aliipatia timu yake bao la pili katika dakika 89 kwa mkwaju wa penati katika juhudi za kuhakikisha hawatoki na kapu la magoli.

Wakiwa wametangulia Nusu Fainali itakayo pigwa katika mji wa
Warsaw Alhamisi.Swali ni Je watakumbana na Uingereza au Italia wanaocheza Kesho Jumapili Mida ya saa 3:45 usiku katika mechi inayosubiriwa kwa hamu.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top