Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUTOKA BUNGENI:Naibu Spika hajaridhika na majibu ya Mh.Mnyika,anapelekwa kwenye kamati ya Maadili ya bunge



Naibu spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amelipeleka suala la tuhuma za Mhe. Mnyika kwa Mhe. Mwigulu Nchemba katika kamati ya haki na maadili.

Hii ni baada ya Mh. Mnyika kutowasilisha ushahidi wake baada ya siku saba alizopewa na spika wa bunge kupita na Mh. Nchemba kuomba mwogozo.

Naibu spika hajaridhika na majibu ya Mnyika,anapelekwa kwa kamati ya maadili ya bunge.

Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge suala la Mh.Mnyika kumtuhumu Mh.Nchemba kuhusika na kashfa ya EPA wakati Mh.Nchemba akisema wakati kashfa hiyo EPA ikifanyika yeye alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Kwa kuwa muda aliopewa wa siku saba umeshaisha na Mnyika amewasilisha maelezo ya awali na sio ushahidi kama alivyoamriwa hivyo suala hilo limepelekwa kwenye Kamti hiyo ili kutoa maamuzi zaidi.

Katika hatua nyingine Mhe. Ndugai amewataka wabunge kutokuwa na tabia ya kuwatuhumu wabunge wenzao kwa masuala mazito bila kuwa na ushahidi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

1 comments:

hivi inaingia akilini kwamba Mh.Mnyika atawakilisha ushahidi huo Bungeni?yaani mkabithi fisi mbuzi wako akulindie.Hata mtoto mdogo hawezi fikiria kitu cha namna hiyo.Na pia Mnyika si mpumbavu wa kihivyo.Labda wampeleke mahakamani,na nina amini hata huko maakamani hatautoa huo ushahidi bali atashtaki kwa watanzania.

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top