Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MADIWANI WA KIGAMBONI WAMTUHUMU MBUNGE WAO MRADI WA MJI MPYA



DIWANI wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Kibada amesema kauli ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile, kuwa ni miongoni mwa madiwani nne waliohongwa na Waziri wa Ardhi ili kuunga mkono ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni haina athari kwake.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana diwani huyo, Juma Nkumbi alisema kauli ya mbunge huyo inaonyesha ni jinsi gani alivofilisika kisiasa mbele ya jamii.
Alisema kutokana na mbunge huyo kushindwa kwake kutoa ushahidi dhidi ya kauli yake hiyo, moja kwa moja imekidhihirishia chama chake kuwa hakuhusika na kitendo hicho.
Nkumbi alisema mbunge huyo amekuwa akitaptapa, kutafuta umaarufu baada ya kupoteza imani kwa wananchi wa jimbo hilo kutokana na kushindwa kwake kwa makusudi kusimamia kero zao.

Aidha, alisema kauli ya Dk. Ndungulile ni yakutaka kuwachonganisha wananchi wa kigamboni ambao hawapingi mradi huo isipokuwa wanataka tathmini ya mali zao ifanyike kwa kuzingatia haki na walipwe vizuri.
Nkumbi alisema kwa kudhihirisha kuwa mradi huo unakubalika, ni hivi karibuni Wenyeviti wa Mitaa wa jimbo hilo, walimtembelea Bungeni, mbunge wa Temeke, Abasi Mtemvu, ambaye ni mwenyekiti wa Wabunge wa Dar es Salaam na kumwambia kuwa kauli anazotoa, Dk. Ndungulile ni mawazo yake wala hakutumwa na wananchi wa Kigamboni
“Madiwani aliowatumu kuhongwa ni pamoja na Juma Nkumbi (Kibada), Suleiman Mathew (Vijibweni), Albert Luambano (Tungi), na Doto Msawa”alifafanua Nkumbi
Majibizano hayo yamekuja baada ya Dk. Ndungulile kuwatuhumu madiwani hao wanne wa jimbo hilo, wakati wa maswali Bungeni kuwa wamehongwa na Waziri wa Ardhi ili wakubali mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top