Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PROFESA LIPUMBA AITAKA SERIKALI KUZINGATIA HOJA ZA WAISLAMU KUHUSU KATIBA MPYA


Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kuzingatia hoja mbalimbali za waislamu katika mchakato wa katiba mpya ili kumaliza zoezi hili kwa wakati.Amesema kutokana na kutosikilizwa kwa waislamu kuhusu hoja zao dhidi ya uundwaji wa katiba mpya ni kikwazo cha utekelezaji wa zoezi hilo linalotarajiwa kufikia tamati Aprili 26 mwaka 2014.Profesa Lipumba alikuwa akihutubia Kongamano la Waislamu jijini hapa lililoandaliwa na Jukwaa la Katiba Mkoa wa Arusha juzi na kuhadharisha kuwa iwapo hoja hizo hazitazingatiwa itakuwa vigumu kukamilika kwake.“Mchakato wa Katiba Mpya sasa ni miezi 16 na iunatarajiwa kukamilika Aprili 26 mwaka 2014, ni wazi iwapo zoezi litaendelea kukumbwa na malalamiko kama haya ya waislamu itakuwa vigumu kukamilika kwa wakati, na iwapo litakamilika basi hiyo haitakuwa katiba iliyokamilika kwakuwa haitoshelezi mawazp na maoni ya wananchi”Alisema.Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanajitosa katika mchakato wa kutoa maoni bila kukosa ikibidi kwa kurikodi kile wanachokipendekeza ili katiba hiyo itakapokamilika waione iwapo inayo maoni waliyotoa ama maoni hao hayapo waikatae.Alisema mchakato wa kudia kuwepo kwa katiba mpya kulianza miaka ya tisini kupitia chama chake, na hata mwaka 2001 walivamiwa na Polisi wakiwa katika maandamano ya amani wakidai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ambapo alivunjwa mkono na kuporwa saa yake na Polisi.Pia alisisitiza madai yake ya kuwepom kwa Tume huru wakati mchakato wa Katiba mpya haujakamilika kwani iwapo mchakato huo hautakamilika kwa wakati Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 utakuwa na matatizo makubwa.Awali Mwenyekiti wa Jukwa la Katiba Shekhe Mohamed Issa aliwataka Waislamu kujitokeza kwa wingi katika mchakato huo ulioanza hivi karibuni kwani kutoshiriki katika zoezi hilo ni kuzuia maoni yao yasiifikia tume ya katiba.Alisema kwa muda mrefu Waislamu hawajawahi kushirikishwa katika mchakato wa uudwaji wa katiba mpya tangu Tanzania ipate uhuru hivyo ni wakati muafaka wa kushiriki na kwamba wajitume ikibidi kitembea kilomita nyingi kuhakikisha wanashiriki wakiwa na hoja na nguvu.Shekhe Issa akizungumzia Sensa na Watu na Makazi alisema hakuna sababu ya serikali kuwalazimisha waislamu kushiriki kuhesabiwa baada ya kutokuwa na kipengele cha dini ya mtu, kwasababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.Aliwataka Waislamu kutohesabiwa siku hiyo iwapo hakutakuwa na kipengele cha dini, na badala yake waandike milangoni ‘sihesabiwi’ katika milango yao ni kuwa mapumzikoni siku hiyo.
Habari na FuulShangwe.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top