KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia kauli aliyoitoa
mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza silaha nchini.
"Kauli
hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya
siasa inamshinda hivyo awaachie vijana" alisema Nape na kuongeza kwamba
anatambua kuwa uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.
Akizungumza
na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa
wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua
ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza siala kinyemela ni
dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.
Kwa
mujibu wa Nape, Dk. Slaa amesikika akitangaza mjini Morogoro kwamba,
CCM imekuwa ikiingiza siala nchini na kuwapa vijana wazitumie wawapo
kwenye makambi ya Umoja wa Vijana wa CCM.
"Kwanza
huyu Mzee inaonyesha ni jinsi gani ufuatiliaji wake wa mambo ni vinyu,
kutoa madai kwamba tumeagiza siala kinyemela kwa ajili ya makambi ya
vijana wetu, wakati inafahamika kwamba wakati huu CCM imo katika
uchaguzi mkuu hatuwezi kabisa kuandaa wala kufanya makambi ya vijana",
alisema Nape.
"Kutokana
na kauli hizi za uzushi, tunazitaka mamlaka zinazosimamia ulinzi na
usalama kumtaka Dk. Slaa awapatie ushahidi wa kina kuhusu mtu au tasisi
yoyote ambayo inaingiza silaha nchini kinyemela, na kama ushahidi wake
utawezesha kupatikana yeyote basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria",
alisema.
"Huyu
Mzee imekuwa kawaida yake kuandaa uongo kila anapoona kwamba anakabia
kushindwa katika operesheni au mipango yake au ya Chama chake kisiasa.
Wakati ule wa Uchaguzi mkuu, alipoona kwamba atashindwa, alizusha kwamba
CCM imeingiza kura nchini kutoka nje ya Nchi, lakini ikabainika kuwa ni
uzushi", alisema.
Alisema,
hatua ya Dk. Slaa kuzusha uongo ni njama ya kuandaa fujo zitakazofanywa
watu walioandaliwa na Chadema, kufanya fujo mitaani wakati wa mikutano
wa chama hicho mkoani Morogoro. " sasa anatoa uongo huu, ili watu wao
waliokusanya watakapofanya fujo azushe kwamba ni vijana waliotumwa na
CCM".
Chama cha Mapinduzi na CHADEMA kwa siku za karibuni vimekuwa katika malumbano makali likiwemo lile la Nape kuishutumu CHADEMA kuwa wanaanda tafrija za kukusanya michango kumbe wana wahadaa Watanzania hivyo wataje mabilioni wanayo pewa na wafadhili toka nchi za nje hali iliyojibiwa vikali na Mnyika wa CHADEMA
Post a Comment