Mhe.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nchini jioni hii mara baada ya
kuhudhuria Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu uliofanyika
kuanzia tarehe 7 hadi 8 Agosti, 2012 mjini Kampala, Uganda. Agenda kuu
ya Mkutano huo ilikuwa ni kutafuta njia ya amani ya kusuluhisha mgogoro
unaondelea Mashariki ya nchi ya Kongo DRC. Rais Kikwete alipokelewa na
Mhe. Bernard K. Membe (MB) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Dkt. Didas Masaburi, Meya wa jiji la Dar es
Salaam kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha, Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (MB). (Picha na Freddy Maro)
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment