Kiongozi wa CHADEMA ambae jina lake halikufamhamika maramoja akiwa ndani ya gari ya polisi FFU baada ya kukamatwa huku akiwapungua mkono wanachama wake .
Vijana wawili wakiwa wameshika bango likiwa ni mmojawapo ya mabango waliyobeba vijana wengi walikuwa wanaelekea kwenye Mkutano mkubwa wa CHADEMA unaofanyika jioni hii mjini Morogoro.
Gari la Polisi nyuma likilifuatilai gari la matangazo la CHAEMA lililokuwa likiwahamasisha watu kujitokeza kwenye mkutano leo hii Mjini Morogoro ambapo CHADEMA wanafanya mkutano mkubwa wa M4C.
Moshi wa mabomu ya kutoa machozi ukiwa umetapakaa kila mahala baada ya purukushani ya utupaji mabomu hayo kwa wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wanaelekea kwenye mkutano wao leo.
Askari hao wa FFU hapo wanawahi wasiachwe baada ya kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA na gari inaanza mwendo
HAPO dhahama ikawakumba waliokuwepo na wasiokuwepo kina mama hawa nao wakajikuta katikati ya vurugu hizo hivyo nao kujikuta wahanga hapo wanajaribu kujiokoa na moshi huo huku kanga nayo ikidondoka na mtoto akiangua kilio kutokana na moshi huo wa mabomu.
M4C kazi ipo hapa kwani licha ya mabomu hayo lakini walijikusanya na kuelendelea tena kuandamana kuelekea kwenye eneo la Mkutano.
Polisi sasa wakiyasindikiza maandamano hayo ya vijana waliokuwa wanaelekea kwenye Mkutano Mkubwa wa CHADEMA unaofanyika muda huu huko mjini Morogoro.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
MHE Mnyika:Msimamo wangu vurugu,risasi,kujeruhi na “kuua” Morogoro!
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio
la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti
fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia
hatua ya kukiona kama chama cha mauaji. Raia watatu wasio na hatia
wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya
amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu
zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video. Vyanzo
vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar
Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi
wamekusanyika kwa wingi hivi sasa. States captured by grand corruption of the
ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping
M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko
kwa maslahi ya wengi.
John
John MNYIKA,
27
Agosti, 2012
Post a Comment