Mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mshariki na kati kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club leo imepongezwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo.
.................................
Akiongea katika Ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania mh, Anna Makinda alisema anawapongeza wachezaji na viongozi wake wote, kwa kulilteta Taifa ubingwa huo ambao timu 11 kutoka nchi wanachama zilishiriki.
Mh Makinda alisema anafuraha siku ya leo, kwa kuwa Bunge limetembelewa na wageni wengi, wakiwemo watu mashuhuri na wageni maalumu timu ya Young Africans Sports Club.
Spika alianza kwa kuwatambulisha Bodi ya Wadhamin wa klabu ya Young Africans wakiongozwa na mama mlezi wa klabu hiyo, Mama Karume, Francis Kifukwe kisha akawatambulisha Mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuph Manji na makamu mwenyekiti ndugu Clement Sanga.
Baada ya hapo ilifuata zamu ya wachezaji na viongozi wakiwa na wazee wa klabu hyo, makofi mengi mfululizo zaidi ya dakika moja vilianza kupigwa kwenye meza baada ya Nahodha Nadir Haroub Cannavaro kusimama na kuonyesha Kombe kwa watu wote na wabunge waliokuwepo ndani ya bunge.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya wabunge na mawaziri baada ya utambulisho wa Young Africans ndani ya bunge, walitoka nje kwa pamoja na kupiga picha na wachezaji na viongozi wa yanga wakiwa na kombe hilo la Kagame.
Baada ya utambulisho, wabunge wa wanachama wa Young Africans waliaaalika wageni wao wote kupata kifungua kinywa katika mgahawa wa bunge.
Wabunge wanachama wa Young Africans waliandaa kikao cha mda mfupi ndani ya ukumbe wa bunge la zaman (Msekwa Hall) ambapo wabunge, viongozi na wachezaji waliweza kufahamiana kwa undani zaidi.
Mwenyekiti Yusph Manji alifungua rasmi tawi jipya katika eneo la Bunge ambapo mwenyekiti wa Yanga tawi la bungeni ni mh. misanga, katibu mkuu wake akiwa ni Mh Godfrey Zambi, mweka hazina mh.Martha Mlata huku Grace Kiwelu, Mwigulu Nchemba, Faki Makame, na wengineo wakitajwa kama wajumbe katika uongozi huo.
Mh Captain George Mkuchika ambaye jana aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamin wa klabu, pia ndio aliyeteuliwa kuwa mlezi wa tawi la Young Africans bungeni.
Dua za kubariki tawi hilo zilisomwa kwa pande zote mbili za dini kisha wabunge na viongozi kupiga picha za pamoja, ambapo pia jioni ya leo wabunge wameaanda futari kwa ajili ya wageni hao.
Timu inatarajiwa kureje jijini Dar kesho kuendelea na maaandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza septembe mosi.
Via Yanga
Post a Comment