Nikamkumbusha kuwa wenzetu wamezindua kwa mara ya kwanza MOVEMENT FOR CHANGE au M4C mwaka 2012, nikamwambia nani kamuiga mwenzake?
Jambo la mwisho nililomjulisha ni kuwa CUF kuzindua V4C na kuendeleza ujumbe wa mabadiliko na CHADEMA kuzindua M4C kwa malengo hayohayo ni utaratibuwa kawaida tu kuuandaa umma kutokukichagua CCM mwaka 2014.
Baadhi ya Vyombo vya habari viache chokochoko na kutaka kudanganya baadhi ya vyama ati vimeshashika dola. CUF na CHADEMA kwa huku bara bado ni wapinzani tu, hata kama tukijidai hatujuani, hata kama tukipeana majina mapya ya ujanja ujanja, ukweli ni kuwa CCM ndiyo wanaongoza dola huku bara na tukishangaa wananchi wataendelea kuumia chini ya mikono ya CCM.
Juhudi za kila chama kujipanga na kuchukua viti zaidi BUNGENI, KWENYE MABARAZA YA MADIWANI, VIJIJI, VITONGOZI NA MITAA, na kupata kura zaidi ndiyo njia ya pekee tuliyonayo hivi sasa baada ya ile ya ushirikiano kushindikana.
Vyama vijipange zaidi na tusipoteze muda wa kutafuta nani kamuiga nani. Siku zote CUF huigwa.
Post a Comment