Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LEMA :SEREKALI ISITUGOMBANISHE CHADEMA NA WAMACHINGA ARUSHA


Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini  Bwana Lema akiongea na waandishi wa habari jana baada ya kuahirisha mkutano wa M4C
 Jemsi ole milya akiongea katika mkutano huo ambapo alisisitiza na kuitaka serekali irejeshe viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na CCM kwani viwanja hivyo vimejengwa kwa kutumia fedha za wananchi na sio za chama hicho ,ambapo alitaja baadhi ni pamoja na kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid,Nyamagana kilichopo mwanza pamoja na kiwanja cha CCM kirumba.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, 

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema amemtaka Mkuu wa Willaya ya Arusha Mjini Bw John Mongela kuhakikisha kuwa anatumia busara zaidi  ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kupitia kwa Mkuu huyo wamegeuza matumizi ya uwanja ambao ulikuwa unatumiwa na CHADEMA kwa ajili ya mikutano ya nje na kuwapa  eneo hilo wa Machinga siku moja kabla ya kufanya mkutano wa hadhara.


Bw Lema aliyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari  mara baada ya chama hicho kushindwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya NMC ambavyo vimegeuzwa kwa ajili ya matumizi ya Wamachinga

Aidha Bw Lema alifafanua kuwa kitendo hicho cha kubadilishiwa matumizi ya uwanja ambao ulikuwa ukitumiwa sana na Chadema umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha na hayo yote yanatokana na chuki binafsi za maslahi ya kivyama ingawaje bado chama hicho kina uwezo mkubwa sana wa kuendelea kufanya kazi yake

Alifafanua kuwa hali hiyo ya kubadilisha matumizi ya uwanja  kutoka uwanja wa matumizi ya kijamii na kwenda kwenye uwanja wa kuuza vitu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo(MACHINGA) umetokana na chuki ambazo zilikuwa zimeelekezwa kwa chama hicho dhidi ya wamachinga hali ambayo imetokana na chuki za siasa hasa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha

“inaamanisha nini leo tumeshapanga kufanya mkutano alafu Mkuu wa Wilaya anaelekeza watu wamwage Vifusi kwa ajili ya eneo la Machinga je wakati wote huo walikuwa wapi  na kama sio kutogombanisha na Machinga ni nini lakini bado tuna nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya mikutano hata kama ni nyumbani kwetu na tutawatetea hawa vijana ambao ni machinga kufa na kuzikana”aliongeza Bw Lema

Pia aliishauri Serikali kuhakikisha kuwa kabla hawajafikiria kuwatoa wafanyabaishara wadogowadogo (MACHINGA)wanatakiwa kutengeneza miundombinu imara ambayo itatumika lakini kwa sasa ndani ya eneo hilo
ambalo limegeuzwa matumizi yake na Mkuu wa Wilaya bado walengwa watapata shida sana na kutokana na hali hiyo hata uchumi nao utadidimia sana

“ukingalia sana ndani ya viwanja hivi vya NMC ambavyo vilikuwa vikitumika na Chadema na sasa ni viwanja vya machinga bado ni hafifu sana kutokana na kuwa hakuna miundombinu yoyote alafu pia kabla hawa watu hawajapelekwa  kule walitakiwa kuhakikisha kuwa wanaboresha ila wamewakimbizia huko kwa ajili ya mkutano wetu  ambao ulikuwa wa kuchakaza sura ya Arusha kutokana na ukweli ambao sisi tunaujua”aliongeza Bw Lema


Awali Katibu wa chama hicho kwa mkoa wa Arusha bw Amani Golugwa  alisema kuwa mbali na hayo wamejipanga kuhakikisha Mji wa Arusha unakuwa na historia yake kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake ya msingi na wala sio kuonewa na baadhi ya viongozi ambao hawana maadili ambao ndio chanzo kikubwa sana cha umaskini.

Chanzo:Arusha Yetu Blog

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top