Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MACHINGA WACHARUKA ARUSHA


 Pichani, wananchi wa Arusha (wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga) wamama, wababa, na vvijana wakionekana kujigawia vijisehemu vya kufanyia biashara mapema leo asubuhi baada ya kufanikiwa kuvamia eneo lililo jirani na soko la Kilombero na kuvunja uzio.

Pichani,Vikosi vya askari Polisi vikiwa tayari tayari kiulinzi. Tangia kuanza kwa zoezi la uvamizi Polisi hawa walikuwa pembeni wakiangalia vurumai hizo bila kuwazuia wananchi hao walioonekana kuwa wengi sana, wenye hasira na umoja. Pengine ni busara imetumika na jeshi la Polisi kuepusha vurugu kuwa na madhara zaidi.

Hatua hiyo inaelezwa ilichangiwa na kitendo cha Manispaa kuwaondoa wafanyabiashara wote waliokuwa wakifanya shughuli zao nje ya soko la Kilombero ambao walielezwa kuwa walipaswa kuhamia eneo jipya la NMC Unga Ltd.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya machinga waliozungumza na Blog hii wanasema kilichowakasirisha na kuamua kuvamia eneo hilo na kujigawia maeneo ni kitendo cha mgambo wa manispaa kuwakamata asubuhi ya leo na kuwatoza faini ya elfu 50 huku wakitakiwa waondoke maeneo ya nje ya soko na kuhamia NMC ambako wamedai tayari kumejaa.

Blog hii iliweza kushuhudia umati wa watu ambao kimsingi hawawezi kueneo eneo jipya la NMC walikogawiwa hivi karibuni ambako tayari kuna vibanda kiasi cha watu wengi kufanyia biashara zao nje ya uzio uliowekwa!


Eeno lililovamiwa hii leo linaelezwa kuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Manispaa na mmiliki wake ambae anaelezwa kutokuwa mmiliki halali. 

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top