Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwan wa Tanzania Bara inaingia raundi ya sita wikiendi hii kwa mechi saba.
Kesho (Oktoba 6 mwaka huu) African Lyon itakuwa mwenyeji wa Azam Fc ''wana lamba lamba'' katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo Ruvu Shooting itaikaribisha Coastal Union ya Tanga''wagosi wa Tanga'' katika mechi itakayochezeshwa na Muamuzi Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
Jumapili (Oktoba 7 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya wekundu wa Msimbazi Simba na Oljoro JKT itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Simba waliotoka sare ya 1-1 na Yanga Wanatakiwa kushinda ili waweze kuendelea kung'ara kileleni mwa Ligi.
Huko Kaitaba kutakuwa na vute nikuvute kati ya wenyeji Kagera Sugar wakatakao wakaribisha Yanga (Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba).Yanga wanahitaji kushinda mechi hiyo ili waweze kupunguza pengo la pointi kati yake na mtani wake Simba wanaoongoza Ligi wakiwa na tofauti ya pointi Tano.
Mgambo Shooting wanao buruza mkia watapambana na Polisi Morogoro (Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga) walio na pointi mbili mpaka sasa, Toto Africans na JKT Ruvu (Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza) na Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya).
Marejeo ya Habari:
Taarifa toka TFF.
Post a Comment